UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI VIZIWAZIWA KWA FEDHA YA SEQUIP WAFIKIA ASILIMIA 75
Na Byarugaba Innocent, Kibaha
Kiasi cha fedha kiasi milioni 470 kutoka Mpango wa maendeleo ya Elimu Sekondari (SEQUIP) zinatarajia kukamilisha ujenzi wa miundombinu inayotakiwa kuanzisha shule mpya ya Viziwaziwa kwenye hiyo, halmashauri ya Mji Kibaha.
Mhandisi wa Mji Kibaha John Alexander amebanisha miundombinu inayojengwa kuwa ni Madarasa 8,Maabara 3,Jengo la utawala,Maktaba,mnara wa kuweka tenki la Maji pamoja na matundu 20 ya vyoo na kwamba ujenzi wake umefikia 75 asilimia.
Aidha fedha hiyo itanunua Komputa moja kwa ajili ya kuchagiza somo la TEHAMA amesema Mhandisi Alexander
Kaimu Ofisa Elimu Sekondari Zakaria Maganga amesema lengo la kujenga shule hiyo kwa kutumia fedha za SEQUIP ni kutokana na Kata hiyo kutokuwa na shule ya Sekondari hivyo imekuwa ni suluhisho la kupunguza umbali kwa wanafunzi waliokuwa wakitembea zaidi ya KM 14 kwenda kufuata masoko shule ya Zogowale au KM 16 shule ya Miembesaba.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amemshukuru Mhe.Samia Suhuhu Hassan na Serikali yake kwa kuendelea kuwajali wananchi wa Kibaha kwenye sekta ya Elimu huku akitoa rai kwa Wazazi na walezi kuwahamasisha watoto wao kusoma kwa bidii hasa masomo ya sayansi ambayo yameendelea kuwa na wataalam wachache nchini.
Wizara ya Elimu,Sayansi na teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Mpango wa miaka 5 (2020-2021/2024-2025) kwa ajili ya kuboresha Elimu ya Sekondari Tanzania hasa kwa kuweka Mazingira mazuri ya kujifunzia ili kutoa Elimu Bora,kuwajengea uwezo walimu ili wawe na mbinu Bora za ufundishaji,kufundisha kidigitali hasa kwenye masomo ya Hisabati na Sayansi pamoja na kujenga shule za Sekondari jirani na Makazi ya wananchi.
Haki Zote Zimahifadhiwa