Na Byarugaba Innocent,Kahama.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Kibaha wamefika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kujifunza namna ya uwezeshaji wa tija kwa Makundi ya akina Mama,Vijana na watu wenye ulemavu ambao ni wanufaikaji wa asilimia kumi ya Mapato ya ndani
Awali akiutambulisha ujumbe uliotoka Kibaha,Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amebainisha lengo la ziara kuwa ni kuona shughuli za makundi hayo yanavyofanya kazi kwa tija kutokana na mikopo ya asilimia kumi ili watapo waambia Vijana wa Kibaha kuwa Vijana wa Kahama wameweza kutengeneza bidhaa,Wana masoko makubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na tayari wameanza kutoa ajira kwa Vijana wenzao wawe na uhalisia usio kuwa na shaka.
Amri Abdul Katibu msaidizi wa wamachinga Manispaa ya Kahama amesema kuwa "Vijana tumekuwa wasikivu,tunaishukuru Serikali yetu kwa kutuwezesha.Tulianza kwa ugumu,mitaji ilikata,lakini tulivumilia,tukanyanyuka na leo tunatengeneza fedha na kupata faida" alisema na kuongeza
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba kando ya kuwapongeza Vijana kwa uaminifu,uzalendo na uthubutu wao ametoa rai kwa Vijana hao kutengeneza bidhaa zao zenye ubora wa umaliziaji ili ziweze kushindana zaidi kwenye Soko la Dunia
Kwa upande wake Mchumi wa Manispaa ya Kahama Florah Sangiwa amesema kuwa tayari Vijana 2754 wameajiriwa kupitia mikopo hiyo na Manispaa imewatengea eneo lenye Ukubwa wa ekari 2160 kwenye eneo maalum lijulikanalo kwa Ummy Mwalimu Industrial Park umbali wa kilomita 3.4 kutoka Barabara kuu ya Tinde na tayari wameshaweka miundombinu ya Barabara,Maji na Umeme kuruhusu shughuli za wanufaikaji hao
Kwa kauli moja Waheshimiwa Madiwani wamempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba kwa utendaji wake mzuri kwani sasa Manispaa ya Kahama imekuwa kama chuo kwa maeneo mengine kufika hapo kujifunza
Wengine waliofuatana na Waheshimiwa Madiwani ni Viongozi wa Chama cha Mapinduzi,Viongozi wa Wamachinga Pwani na Wataalam wa Halmashauri.
Haki Zote Zimahifadhiwa