• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI MKUU:SERIKALI IMESAJILI MIRADI YA UWEKEZAJI 537.

Posted on: April 24th, 2023

 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021 hadi Januari, 2023 Serikali ilisajili jumla ya miradi ya uwekezaji 537 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 7,222.

 Amesema hayo leo Alhamisi (Aprili 20, 2023) alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki, kinachojengwa na Kampuni ya East Africa Commercial and Logistics Center kwenye eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

 Amesema kuwa, hatua hiyo imetokana na kuboreshwa kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kuimarisha Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja ili kuvutia wawekezaji kwa kupunguza kero na kurahisisha utoaji huduma.

Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa ongezeko la usajili wa miradi hiyo unatarajia kutoa  ajira takriban 92,770 “Kiwango hiki ni kikubwa kuwahi kuandikishwa katika kipindi chochote tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961”

 Amesema kuwa, Serikali kupitia Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA)  imefanikiwa kusajili Miradi 38 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 139.70 na mauzo nje yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 191.04.

 “Miradi hiyo ni mahsusi katika sekta zinazozalisha bidhaa zitokanazo na Kilimo, bidhaa za viwandani, bidhaa za Mifugo, bidhaa za Kemikali, bidhaa za madini na bidhaa za misitu”

 Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu sahihi ya uwekezaji, na  kuleta mitaji yao “tunayo mazingira mazuri ya uwekezaji”

 Akizungumzia kuhusu Mradi wa Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kituo hicho kitakuwa na maduka zaidi ya elfu mbili, ambayo yatakuwa na ukubwa tofauti tofauti hivyo kuweza kukidhi mahitaji ya wafanyabishara wa aina tofauti tofauti “Kutokana na ukweli huo, mtakubaliana nami kuwa kituo hiki kitapanua fursa ya Watanzania wengi kufanyabiashara katika eneo hili”

Amesema kuwa kituo hicho pia kitatoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo almaarufu Wamachinga kufanya biashara zao katika eneo la nje baada ya kusitisha shughuli za kituo hiki kila siku.

“Kitendo hiki ni cha kizalendo kwani kitatoa fursa kwa Watanzania wenye kipato cha chini ambao hawatakuwa na uwezo wa kupata vizimba ndani kunufaika na uwepo wa kituo hiki kwa kuweka biashara zao nje kwa muda watakaopangiwa”

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Angellah Kairuki amesema kuwa mradi huo unathamani ya dola za Kimarekani milioni 81.827

Amesema kuwa Mradi huo utaifungua Tanzania kibiashara na kukuza uchumi kutokana na biashara zitakazokuwa zikifanyika na kukuza mahusiano ya Kimataifa kwa kuwa na muingiliano wa wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.

Ameongeza kuwa kituo hicho kitatoa ajira za moja kwa moja zaidi 15000 na utahamasisha maendeleo ya setka mbali mbali ambazo nazo zitazalisha ajira zisizo za moja kwa moja 50000 hivyo kuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha kwa wananchi wa Tanzania.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya East Africa Commercial and Logistics Center (EACLC) Dkt. Cathy Wang amesema kuwa mapato ya jumla kwa mwaka yatafika zaidi ya dola za marekani milioni 500 pindi mradi huo utakapokamilika hivyo kusaidia katika ukuaji wa pato la taifa na kuongeza mapato ya kikodi.

Amesema kampuni hiyo imedhamiria kujenga mradi huo wa kimkakati ambao utakuwa moja ya mradi mkubwa ndani ya afrika mashariki na utawezesha kukuza biashara ndogo nchini na kupanua biashara hizo ndani ya soko kubwa la Afrika.

Amesema kuwa mradi huo utasaidia kukuza biashara ndogo na kupanuka zaidi ndani ya soko la afrika na utawezesha kuchachusha ukuaji wa uchumi endelevu ifikapo 2025.

Mradi huo utakuwa na maduka 2060 yenye ukubwa wa jumla ya mita za mraba 75000 ambapo eneo hilo litakuwa na huduma zote za kibiashara ikiwemo mabenki na huduma ufungishaji na usafirishaji.

Pia, Mapato ya jumla kwa mwaka yatafikia zaidi ya USD Milioni 500 mradi huo ukiwa umekamilika hivyo kusaidia katika ukuaji wa pato la Taifa la Tanzania na kuongeza mapato ya kikodi.

Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN KIBAHA TOWN UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • TANGAZO LA MNADA WA NG'OMBE KWA WAFANYA BIASHARA WA NYAMA NA NG'OMBE ,MTAA WA MTAKUJA KATA YA PANGANI, UNAOFANYIKA KILA ALHAMISI. March 13, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KIBAHA MANISPAA YANG'ARA UKUSANYAJI WA MAPATO

    April 30, 2025
  • DKT.SHEMWELEKWA ATETA NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KIBAHA Na.Byarugaba Innocent, Kibaha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufa

    November 22, 2024
  • DKT.SHEMWELEKWA ATETA NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KIBAHA Na.Byarugaba Innocent, Kibaha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufa

    November 22, 2024
  • MHE.NDOMBA AZINDUA GARI MPYA AINA YA LANDCRUSER ILIYONUNULIWA KWA MAPATO YA NDANI

    November 21, 2024
  • Tazama Zote

Video

Mh. Waziri Mkuu akiwa ziarani Kibaha
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa