Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Maonyesho ya uwekezaji na biashara Mkoa Pwani yameanza Oktoba 5,2022 na yanazinduliwa rasmi leo Rais wa awamu ya nne Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete.
Maonyesho haya yenye yanayofanyika kwenye Viwanja vya Stendi ya Zamani maili moja yakiwa na kauli mbiu isemayo Pwani ni sehemu sahihi ya uwekezaji,pamoja tujenge Viwanda kwa uchumi na ajira endelevu yatafikia tamati Oktoba 10,2022
Tayari wageni mbalimbali mashughuli wakiwemo Waheshimiwa Madiwani,wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya Mkoa wa wamewasili kushuhudia maonyesho hayo
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde ametoa rai kwa wananchi hususan Kibaha Mjini kuyatembelea maonyesho haya ili kujionea namna Halmashauri ya Mji Kibaha ilivyofanikiwa kwenye uwekezaji na kwamba Sasa bidhaa nyingi za viwandani zinapatikana nchini zikiwa zimetengenezwa au kuunganishwa hapa.
Steve Kadri amesema ni fursa nzuri kwa Mkoa wa Pwani kuandaa maonyesho haya kwani yanapanua wigo wa uwekezaji na biashara na kuongeza mzunguka wa fedha kwenye Mkoa kwani wageni wanapata mahitaji hapa.
Mkoa wa Pwani una wawekezaji kwenye sekta ya Viwanda zaidi ya 1400 ambao wameongeza Mapato ya Pato la Taifa.
Haki Zote Zimahifadhiwa