DC KIBAHA AFUTA UONGOZI WA SOKO LA MNARANI, Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Assumpter Mshama amewasimamisha Ramadhani Maulidi na Ernest Kisandu ambao ni Mwenyekiti na Katibu wa Soko kuu la Mnarani mjini Kibaha.
Aidha, Abdallah Ndauka ambaye ni mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Pwani ameteuliwa kuwa kiongozi wa mpito mpaka hapo uongozi mpya utakapochaguliwa.
Utenguzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji kibaha kilipokuwa kikifanyika kikao kati ya wafanyabiashara na Mkuu wa wilaya kujadili mustakabali wa ulipaji kodi ya pango.
Mshama amesema kuwa viongozi hao wamekuwa hawana msaada kwa Serikali kwani badala ya kuongoza kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi wao wamekuwa sehemu ya migomo na migogoro isiyoisha huku wakiendesha siasa sokoni badala ya biashara. "Kuanzia leo ninyi ni viongozi wastaafu ni bora nipate viongozi wapya wenye nia njema na Serikali badala ya ninyi mnaoendesha Siasa na kuhamasisha migogoro badala ya maendeleo" Alisema.
Uongozi huo upo madarakani tangu 2016.
Haki Zote Zimahifadhiwa