• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TSH milioni 420 ya mapato ya ndani kutengeneza Barabara za mitaa, Wananchi wapongeza

Posted on: October 3rd, 2025

Manispaa ya Kibaha imetoa Tsh Milioni 420 Kutatua Changamoto ya Barabara za Mitaa


KIBAHA: Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imetoa jumla ya Shilingi Milioni 420 kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kutengeneza na kufungua barabara za mitaa katika kata zote za manispaa hiyo, ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya ya miundombinu ya barabara.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, amesema Tayari kata zote Manispaa ya Kibaha zimepokea mgao wa Shilingi Milioni 30 Kwa ajili ya kutekeleza miradi ya uboreshaji wa barabara ili kurahisisha huduma mbalimbali kwa wananchi.


“Kupitia mapato yetu ya ndani, tumeamua kuwekeza katika barabara za mitaa kwa kuwa ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya wananchi. Kila kata sasa ina Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya miradi hii na tutaendelea kusimamia utekelezaji wake kwa karibu,” amesema Dkt. Shemwelekwa.


Katika Kata ya Sofu, wananchi wameipokea kwa furaha hatua hiyo na wamepongeza uongozi wa Manispaa kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kutatua kero ya barabara.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa wa Twendepamoja Mhe Idd Alfan amesema, “Wananchi wamehamasika sana kuona kodi wanazotoa zinatumika moja kwa moja kuboresha maisha yao. Mradi huu umewapa motisha zaidi ya kulipa kodi kwa hiari kwa sababu wanaona matokeo yake.”


Mwananchi wa Kata hiyo, Bi. Deborah Mkoma, amesema barabara zinazotengenezwa ni muhimu sana kwa kuwa zinapitika kuelekea hospitalini na maeneo mengine ya huduma muhimu.


“Kuna sehemu magari yalikuwa hayawezi kufika kabisa kutokana na ubovu wa barabara, lakini sasa hata bodaboda wanafika bila shida na kwa bei nafuu. Tunampongeza sana Mkurugenzi kwa juhudi zake,” alisema Bi. Mkoma.


Wananchi wa Manispaa ya Kibaha kwa ujumla wameonyesha matumaini makubwa kuwa mradi huu utaleta mabadiliko makubwa katika maisha yao ya kila siku na wameahidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye Usajili wa waombaji nafasi ya muda usimamizi wa Uchaguzi Mkuu 2025 October 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Jeshi la zimamoto na Uokoaji laadhimisha siku ya kupunguza majanga Kwa kufanya shughuli mbalimbali

    October 13, 2025
  • TSH milioni 420 ya mapato ya ndani kutengeneza Barabara za mitaa, Wananchi wapongeza

    October 03, 2025
  • Rc pwani aitaka Taasisi ya Elimu ya watu wazima kuleta matokeo chanya Sasa.

    October 02, 2025
  • Wazee 160 Mtaa wa Uyaoni waadhimisha siku ya wazee Duniani Kwa kupima Afya zao

    October 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

Matangazo Mubashara Hafla ya Utiaji Saini mikataba ya Soko la Mnarani na miundombinu ya Barabara
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa