Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Kibaha ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Assumpter Mshama inatarajia kufanya ziara ya kikazi kwenye Kata zote za Halmashauri ya Mji Kibaha ili kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.DK.John Pombe Joseph Magufuli kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa kila Mtanzania.
Ratiba ya ziara hiyo inatarajia kuanza na Kata ya Mailimoja hapo Mei 3, 2018 na itahitimishwa katika Kata ya Mbwawa Desemba 27, 2018 ambapo ina wastani wa mzunguko wa mara mbili kwenye kila kata kwa kata zote kumi na nne (14) zenye jumla ya mitaa sabini na tatu (73) katika Halmashauri ya Mji Kibaha.
Katika ziara hiyo itakayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mh.Asumpter Mshama ataambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Bi. Jenifa Omolo pamoja wa Wataalam kutoka idara na Vitengo vya Halmashauri ya Mji Kibaha.
Bofya Hapa:Ratiba ya Ziara ya Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa ajili ya kusikiliza kero za Wananchi.pdf
<%
Haki Zote Zimahifadhiwa