• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TUENDELEE KUUTHAMNI MUUNGANO WETU-Mhe. Dkt. Selemani Jafo

Posted on: April 8th, 2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Watanzania wana kila sababu ya kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amewataka Watanzania kutembea kifua mbele kujivunia Muungano huo adhimu ambao umeleta faida lukuki zikiwemo uhusiano mzuri baina ya wananchi wa pande zote mbili katika Nyanja mbalimbali.

Dkt. Jafo amesema hayo wakati akizungumza kwenya uzinduzi wa Nembo na Kaulimbiu ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanywa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa jijini Dodoma leo Aprili 08, 2024.

Waziri Dkt. Jafo amewashukuru na kuwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa usimamizi wao na kuwezesha utatuzi wa changamoto 15 kati ya 18 ndani ya miaka mitatu ya uongozi wao.

“Leo hii tunaanza mbio za miaka 60 ya Muungano na hili ni jambo la kipekee tangu Muungano ulipoundwa, mwaka huu nchi yetu inatengeneza historia yake ya kipekee na sisi Ofisi ya Makamu wa Rais yale yote ambayo Watanzania walipaswa kujivunia tumejitahidi kufanya kila linalowezekana,” amesema Dkt. Jafo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma amesema kuwa Muungano ni tunu kubwa hivyo ni wajibu weu kuulinda na kuutunza.

Amesema Watanzania hawana budi kuutetea kwa hali yoyote ile kuhakikisha unaendelea kudumu ili wananchi waishi kwa usalama na Amani.

Mhe. Hamza amewataka Watanzania kuwaenzi Waasisi wa Muungano Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye Aprili 07, 2024 ilikuwa kumbukizi ya miaka 52 ya kifo chake.

Mhe. Waziri Hamza amesema kuwa uzinduzi rasmi wa sherehe za Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar unatarajiwa kufanyika Aprili 14, 2024.

Kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano kinatarajiwa kufanyika Aprili 26, 2024 ambapo kitatanguliwa na shughuli mbalimbali zitakazofanyika Tanzania Bara na Zanzibar.

Kaulimbiu ya sherehe za mwaka 2024 ni ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu’

Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN KIBAHA TOWN UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • TANGAZO LA MNADA WA NG'OMBE KWA WAFANYA BIASHARA WA NYAMA NA NG'OMBE ,MTAA WA MTAKUJA KATA YA PANGANI, UNAOFANYIKA KILA ALHAMISI. March 13, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • ZOEZI LA MABORESHO YA DAFTARI LA WAPIGA KURA KUANZA MEI 16 KIBAHA TC

    May 09, 2025
  • KIBAHA MANISPAA YANG'ARA UKUSANYAJI WA MAPATO

    April 30, 2025
  • DKT.SHEMWELEKWA ATETA NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KIBAHA Na.Byarugaba Innocent, Kibaha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufa

    November 22, 2024
  • DKT.SHEMWELEKWA ATETA NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KIBAHA Na.Byarugaba Innocent, Kibaha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufa

    November 22, 2024
  • Tazama Zote

Video

Mh. Waziri Mkuu akiwa ziarani Kibaha
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa