• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RAS PWANI AWATAKA WATUMISHI KUCHAPA KAZI KWA KASI NA KUZINGATIA WELEDI

Posted on: March 12th, 2021

RAS PWANI AWATAKA WATUMISHI KUCHAPA KAZI KWA KASI NA KUZINGATIA WELEDI 

Na Innocent Byarugaba, Kibaha

Katibu tawala Mkoa wa Pwani, Dkt Delphine Magere amefanya ziara ya siku moja kwenye halmashauri ya mji wa Kibaha kwa lengo la kuhimiza utendaji kazi kwa watumishi huku wakizingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo yote ya utumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi.

Akiwalisilisha taarifa ya watumishi, Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kibaha Jenifa Omolo alisema kuwa ikama ya watumishi ni 2203 hata hivyo waliopo ni 2033 huku kukiwa na upungufu wa watumishi 170. Aidha,  alisema kuwa watumishi 66 watarajiwa kuajiriwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwani tayari mishahara yao imeshatengwa na kuidhinishwa na Ofisi ya Raisi-Utumishi na utawala bora.

Akiongea na watumishi kwenye ukumbi wa halmshauri, Dkt. Magere alitumia fursa hiyo kuwasilisha salaam kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo sanjali na kuwatakia mwaka mpya 2021 na kuwapongeza watumishi wote kwa kufanikisha ufaulu mkubwa kwenye mitihani ya kitaifa, ukusanyaji wa mapato, Viwanda na sekta nyingine kwani mafanikio hayo yanaonesha kweli halmashauri ya Mji Kibaha ni Makao makuu ya Mkoa wa Pwani huku akitoa rai ya kutojibweteka kwa mafanikio hayo zaidi ya kuongeza kasi zaidi kiutendaji.

Katika mkutano huu changamoto za watumishi ziliibuka.  Juma Mkalipa na Mkaminoela Hangaya waliotaka kujua ni lini serikali itaboresha masilahi ya watumishi hasa kuongeza Mishahara na kulipa malimbikizo ambayo serikali haojalipa kwa muda mrefu

Akijibu changamoto hizo, Dkt.Magere aliwasihi watumishi wote kuwa watulivu na wavumilivu kwani serikali yetu inayoongozwa na Mheshimiwa  John Pombe Magufuli ni sikivu na kwamba itaongeza muda ukifika kwani kwa sasa serikali imejikita kwenye kujenga  uchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu na itakapokamilika suala hilo litatazamwa na kwamba hii sio Pwani tu ni nchi nzima

Akihitimisha mkutano Dkt.Magere aliwasihi watumishi kuongeza kasi ya uwajibikaji kwa kupendana, kutokufanyakazi kwa mazoea, kutenda kwa ubunifu utakaoongeza tija, kubuni vyanzo vipya vya mapato na kushiriki vyema kwenye ukusanyaji wa mapato huku mianya ya rushwa na upotevu ikizibwa. Aidha, amewataka watumishi kutolaumiana na kunyoosheana vidole kwenye uwajibikaji huku akisisitiza kuheshimiana na kuvumiliana kwani hakuna binadamu aliyemkamilifu mbele za mwenyezi Mungu.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022 February 03, 2021
  • SHILINGI 249,240,000/ KUKOPESHWA KWA VIKUNDI 76 MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE,VIJANA NA WALEMAVU KIBAHA MJI February 17, 2021
  • UUZAJI WA VIWANJA HALAMASHAURI YA MJI KIBAHA March 12, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA HALI YA UFAULU KWENYE MITIHANI YA KITAIFA YA KIDATO CHA IV, KIDATO CHA II, DARASA LA VII NA DARASA LA IV HALMASHAURI YA MJI KIBAHA, 2020 March 12, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAS PWANI AWATAKA WATUMISHI KUCHAPA KAZI KWA KASI NA KUZINGATIA WELEDI

    March 12, 2021
  • JPM KATUJENGEA HOSPITALI YA WILAYA ….. TWENDENI KUTIBIWA

    March 08, 2021
  • RC–PWANI JEMBE LINALOTATUA KERO ZA WANANCHI KWENYE MAENEO YAO YA KUJITAFUTIA RIZIKI

    March 02, 2021
  • HOSPITALI YA WILAYA KIBAHA MJI YAPATA MASHINE YA MIONZI

    March 01, 2021
  • Tazama Zote

Video

Mh. Waziri Mkuu akiwa ziarani Kibaha
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

    Kibaha Town Council

    Anuani ya Posta: P.0.Box 30112

    Simu: 023 240 2938

    Simu ya Kiganjani: Mkurugenz0715390421

    Barua Pepe: td.kibaha@pwani.go.tz & td@kibahatc.go.tz. SIMU: Afisa Mipango Miji: 0754002729 & Afisa Ardhi: 0767506970

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa