MAJUKUMU YA MKUU WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
- Kuiwakilisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika Halmashauri kuhusu masuala ya Elimu ya Sekondari.
- Kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sheria na Kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu ya sekondari.
- Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu masuala yote ya elimu ya sekondari.
- Kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari katika Halmashauri
- Kusimamia haki na maslahi ya walimu na watumishi wengine wa ngazi ya elimu sekondari katika Halmashauri.
- Kusimamia na kudhibiti akaunti ya elimu ya sekondari na kuahakikisha kuwa fedha za elimu ya sekondari zinatumika kama ilivyokusudiwa.
- Kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu sekondari
- Kufuatilia na kuthimini maendeleo ya elimu ya sekondari katika Halmashauri.
- Kuhakikisha kuwa shule zote za serikali katika Halmashauri zinainua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia ikiwa ni pamoja na utunzaji wa madarasa, madarasa, nyumba za walimu, maabara, maktaba na vyoo.
- Kusimamia tathimini ya wazi ya utendaji kazi (Open Performance Review and Appraisal System - OPRAS) kwa walimu na watumishi wa sekondari.
- Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu , watumishi na wanafunzi wa shule za sekondari katika Halmashauri na kufanya kazi nyingine kama utakavyoelekezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri.
Kibaha Town Council
Anuani ya Posta: P.0.Box 30112
Simu: 023 240 2938
Simu ya Kiganjani: Mkurugenz0715390421
Barua Pepe: td.kibaha@pwani.go.tz & td@kibahatc.go.tz. SIMU: Afisa Mipango Miji: 0754002729 & Afisa Ardhi: 0767506970
Haki Zote Zimahifadhiwa