TANGAZO MAALUM
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI KIBAHA, ANAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MITAA YA MAILIMOJA NA TANGINI KUACHA MARA MOJA SHUGHULI ZA UENDELEZAJI/UJENZI WA MAENEO YAO ILI KURUHUSU ZOEZI LA PAMOJA LA KURASIMISHA ARDHI NA KURORESHA MAKAZI YA WANANCHI HAO KUENDANA NA MPANGO KAMAMBE WA MJI WA KIBAHA.
HII NI KATIKA KUTEKELEZA SHERIA YA MIPANGOMIJI NAMBA 8 YA MWAKA 2007 YA KUSIMAMIA UENDELEZAJI NA MATUMIZI BORA YA ARDHI.
WANANCHI MNAOMBWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WATAALAM WATAKAOSHIRIKI KATIKA KAZI HIYO KWA LENGO LA KUTEKELEZA SERA YA TAIFA YA UENDELEZAJI MAKAZI YA MWAKA 2000
LIMETOLEWA NA;
MKURUGENZI WA MJI
HALMASHAURI YA MJI KIBAHA
Haki Zote Zimahifadhiwa