Zoezi la maboresho ya Daftari la Wapiga Kura Kuanza Mei 16 Kibaha Tc
Afisa Mwandikishaji jimbo la kibaha mjini alikua na kikao na wadau wa Vyama vya siasa kujadili maandalizi ya Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Awamu ya pili pamoja na uwekaji wazi Daftari la Uboreshaji awamu ya kwanza.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti ametoa wito kwa Vyama hivyo kwenda kuwahamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo, hususan wale ambao hawakubahatika kuboresha taarifa zao awali, Ameeleza kuwa ni muhimu kwa Wananchi ambao taarifa zao zilikua na makosa au waliohama makazi kujitokeza katika Vituo husika kwaajli ya kufanya marejebisho.
Zoezi linaanza tar 16-22/5/2025 kwa muda wa siku saba.
Haki Zote Zimahifadhiwa