DKT.SHEMWELEKWA ATETA NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KIBAHA
Na.Byarugaba Innocent, Kibaha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufanyabiashara kihalali na kulipa Kodi ya Serikali kwa wakati.
Awali Afisa Mipango na uratibu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Faraja Lucas Maliga amesoma Mapato yanayokusanywa kwenye vituo vyao kuhuku akianisha Matumizi yake kuwa kuwahudumia wananchi kwa Kujenga Shule, Hospitali,Vituo vya afya, kuchonga barabara na mengineyo huku akitoa rai kulipa Kodi wanazostahili kwa wakati.
Wawakilishi kwa niaba ya Wafanyabiashara wengine ni Negero na Admire wamesema kuwa wamefurahishwa na utaratibu Mpya wa Mkurugenzi Dkt. Shemwelekwa kuwatambua na kuwaita kubadilishana naye uzoefu kibiashara na kwamba amelenga kuboresha biashara zao.
"Nawasihi sana,nipeni ushirikiano ili sote tukishirikiana tupate Mapato yatakayo hudumia wananchi. Tukiungana kukusanya Mapato,tunakwenda kuibadili Kibaha Kimaendeleo"amesema Dkt.Shemwelekwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon John ametoa vyeti Maalum kwa kampuni ya Admire na National oil kutambua wepesi wao wa kulipa Kodi kwa wakati.
Haki Zote Zimahifadhiwa