Halmashauri ya Mji Kibaha ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 750 sawa na ekari 185,276. Kati ya hizo ekari 13,805.27 ni kwa matumizi ya viwanda. Maeneo hayo ni Vikawe ekari 454.6, Mbwawa ekari 3,560.51, Mailimoja ekari 208.15, pembezoni mwa barabara ya Morogoro ekari 1,020.75, Miomboni ekari 34 na Zegereni ekari 8,527.26
Eneo la viwanda vikubwa lipo Zegereni Kata ya Misugusugu umbali wa kilomita 4.5 kutoka barabara kuu iendayo Morogoro kutokea Dar es Salaam, eneo hili lina ukubwa wa Ekari 1,246.64
Hadi sasa Halmashauri imepima viwanja vipatavyo 119 katika eneo lenye ukubwa wa ekari 669.72. Aidha, zoezi la upimaji kwa Kiaha mjini ni endelevu. Kati ya viwanja hivyo, 59 vimemilikishwa kwa wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Katika eneo la Zegereni viwanda 7 tayari vinafanya kazi za uzalishaji wa Nondo, Asali, Gypsum, Kuchakata Oil chafu ili kupata vilainishi, kutengeneza nguzo za zege, Vipodozi na kusindika unga wa mahindi na chakula cha mifugo
Aidha, viwanja vilivyomilikishwa ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za uendelezaji ni pamoja na Kairuki Pharmacetical Industry Ltd, Bohari Kuu ya Madawa (MSD), Budget Movers, Jafra Investment & Suppliers Ltd, Bhari Pharmacy Ltd na Darworth Group.
Ushiriki wa Halmashauri ya mji wa Kibaha katika uwekezaji wa viwanda ni pamoja na kushughulikia na kuwezesha upatikanaji wa maeneo, upimaji viwanja kwa matumizi ya viwanda, utoaji wa hati miliki pamoja na vibali vya ujenzi ndani ya muda mfupi, kuhakikisha uwepo wa miundombinu wezeshi katika maeneo ya viwanda kama barabara, ambapo Halmashauri imechonga barabara ndani ya eneo la viwanda
Viwanda hivi vimeweza kutoa ajira zipazo 1,101 kwa mikataba katika fani mbalimbali kwa wakazi wa ndani na nje ya Mji wa Kibaha na vibarua wapatao 466. Aidha, inategemewa kuwepo na ongezeko zaidi la ajira pindi uendelezaji wa viwanda vyote utakapokamilika na kufanya kazi.
Halmashauri imeweza kusimamia uendelezaji wa ardhi unaozingatia matumizi bora ya ardhi na kuongeza mapato ya ndani kwa kiasi cha shilingi Bilioni 1.759 kwa mwaka wa fedha 2017/18.
“Tanzania ya Uchumi wa Viwanda inawezekana shiriki sasa katika ujenzi wake”.
Jenifa C. Omolo
Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya MjiKibaha
Karibuni Kibaha Mji kwa Uwekezaji
Haki Zote Zimahifadhiwa