Na Innocent Byarugaba,Kibaha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameidhinisha kiasi cha fedha shilingi 760 milioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 38 vya Madarasa kwa Halmashauri ya Mji Kibaha vitakavyowanufaisha wanafunzi 3946 wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza Januari,2023.
Afisa Elimu Vifaa na takwimu wa Halmashauri Optuna Kasanda amesema uhitaji wa Madarasa ilikuwa 41 hata hivyo amemshukuru Mhe.Rais kwa kuidhinisha kiasi hicho cha Madarasa kwani kitapunguza tatizo kwa asilimia 93
Ameongeza kuwa jumla ya wanafunzi wa kike 1656 na wanafunzi wa kiume 2290 wanatarajia kunufaika na vyumba hivyo na kwamba kwa uwiano huo Madarasa yatawatosheleza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema jumla ya shule 12 zimenufaika na Mpango huo na kwamba sehemu ya fedha hizo zitagharamia samani.
Mhandisi Munde amebainisha kuwa ujenzi utafanyika kwa muda wa siku 75 kuanzia Oktoba mpaka Disemba 15,2022 na kwamba utaratibu utakaotumika ni "Force account"kwa ramani ya Madarasa iliyotumika kwenye utekelezaji wa programu ya EP4R.
Tayari fedha zimeshaingia kwenye account za shule husika kwa utekelezaji.
Haki Zote Zimahifadhiwa