Na Netho Sichali
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kibaha imetoa huduma bure ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi zaidi ya 200 waliopo katika Halmashauri hiyo na kuhamasisha jamii kufanya mazoezi.
Baadhi ya magonjwa yaliyofanyiwa uchunguzi ni pamoja na ugonjwa wa presha,kisukari na huduma ya kuchangia damu ambapo kati ya hao Wananchi 50 waligundulika kuwa na ugonjwa wa presha na wananchi nane wamegundulika kuwa na ugonjwa wa kisukari.
Afisa afya wa mkoa wa Pwani David Vuo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya afya yaliyofanyika Oktoba 25/2025 katika viwanja vya bwawani vilivyopo Kata ya Tumbi Manispaa ya Kibaha.

