Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Ni takribani siku 730 zinazobeba Miezi 24 sawa na saa 17,520 tu za Dkt.Samia Suluhu Hassan kazini baada ya kifo cha mtangulizi wake Dkt.John Magufuli kuaga Dunia.Hakika yalikuwa majonzi makubwa kwa watanzania kumpoteza Rais aliyekuwa madarakani,hii ni historia mbaya kwa watanzania iliyotokea Machi 17,2021 na hakika haitamaniwi tena.
Tarehe 19 Machi,2021 ilikuwa ni mwanzo wa safari mpya ya Dkt.Samia baada ya kuapishwa na kula kiapo na kuitwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.Safari ni hatua!Sasa anatikiza miaka miwili inatimia hapo Machi 19,2023.Siku hazigandi aisee!
Halmashauri ya Mji Kibaha imesafiri na Rais Samia kwenye kipindi chote hatua kwa hatua.Amefanya mengi Kibaha.Amegusa sekta ya Afya,Elimu,Maji,miundombinu na mengineyo mazuri kwa watanzania.Hata hivyo,kwa leo tumtazame Dkt.Samia alivyoangazia Elimu Sekondari na kuibadili taswira machoni pa wengi.Ni ukweli usiopingika kuwa ameng'amua usemi wa wahenga usema ulimu ni ufunguo wa Maisha.Ufunguo umetua Kibaha.Asante Mama!
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha ameeleza kuwa tayari Bilioni 3,081,000,000.00 zimetua Kibaha Mji.Zimetumika kuiboresha sekta ya Elimu Sekondari.Madarasa 103 yenye thamani ya Shilingi bilioni 2,080,000,000.00 yamekamilika,yanatumika kuboresha uwezo wa ujifunzaji kwa wanafunzi kuinua Kiwango cha taaluma.Aidha,jumla ya Milioni 200,000,000 kuikarabati shule ya Sekondari Tumbi ili kuirudisha kwenye hali ya usasa na ubora zaidi.
Dkt.Samia amedhamiria makubwa kwenye sekta ya Elimu Sekondari.Serikali yake ndani ya kipindi cha miaka miwili imepitisha kiasi cha milioni 470,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Viziwaziwa kupitia mradi wa SEQUIP.Tayari miundombinu ya Madarasa,maabara,majengo ya utawala,maktaba,TEHAMA na mahitaji mengine yamekamilika.Shule ipo mguu sawa kuwapokea wanafunzi na walimu tayari kwa kazi.Kazi Moja tu,masomo kuwapa wanafunzi maarifa mapya.
Ni wakati huohuo milioni 531,000,000.00 zimetumika kujenga miundombinu mingine mathalani;Bwalo,matundu ya vyoo,majengo ya utawala,ofisi za walimu na maabara ili kuweka Mazingira wezeshi ya kutolea Elimu.
Mhe.Nickson Simon,Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amempongeza Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani na kumshukuru kwa kutoa fedha nyingi Kibaha kuimarisha Sekta ya Elimu Kibaha.Aidha,ameahidi kuzidi kumsaidia kusimamia na kwamba amewataka wasaidizi wake waanze kufanya kazi zinazoleta matokea chanya.
Afisa Elimu Sekondari Rosemary Mary msasi amesema majengo haya yamesadia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto za majengo na miundombinu mingine na ameahidi kuongeza usimamizi wa karibu ili yawezekutumika kwa muda mrefu.
Haki Zote Zimahifadhiwa