Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Mei 14, 2025 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya siku moja kwa Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambayo yanahusisha waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kutoka Kata zote za Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani. Zoezi la uboreshaji awamu ya pili linataraji kuanza Mei 16 hadi 22, 2025 sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la Wapiga Kura na vituo vitafunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.
Haki Zote Zimahifadhiwa