Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Mapema leo Oktoba 18,2022 Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha amewaongoza Wakuu wa Idara,Vitengo na Sehemu kwenda 'site' yalipo Machinjio ya Kisasa kuona na kushauri namna sahihi ya kutafuta mwarobaini kwa kuweka Maji ya uhakika yatakayotumika kwenye shughuli za uchinjaji wa wanyama.
Tayari Halmashauri wamekuja na Mipango miwili ya kupata Maji ya uhakika ikiwemo kuchimba Kisima kirefu na kutengeneza miundombinu ya kuvunia Maji ya Mvua yatakayohifadhiwa kwenye matenki maalum na kuwezesha uwepo wa Maji kwa siku zote 365 za Mwaka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema ni fahari kubwa kuwaandalia Kitoweo cha nyama walaji kwenye Mazingira nadhifu lakini bila Maji ya uhakika haiwezekani hivyo ameitaka menejimenti kuweka nguvu kuhakikisha Maji ya uhakika yanakuwepo
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Joseph Njau amesema kwa dalili zilizoonekana kwenye Kisima ambacho kimechimbwa ni wazi shida ya Maji inakwenda kuwa historia hivyo Halmashauri itaokoa kiasi cha fedha kinachotumika kununua Maji wakati huu.
Aidha,ameeleza kuwa mkakati huu kabambe wa kupata Maji ya uhakika utapanua wigo kwa wafanyabiashara wa ndani na nje wa kusafisha nyama kwani tayari Kuna makampuni kadhaa ambayo yameinesha nia ya kutumia machinjio haya.
Haki Zote Zimahifadhiwa