Watendaji wa Kata Manispaa ya Kibaha Katika Ziara ya Mafunzo Jijini Mbeya
Mbeya, Tanzania
Watendaji wa kata kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha wameanza ziara ya mafunzo ya siku tano katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa lengo la kujifunza mbinu bora za ukusanyaji wa mapato, utoaji wa vibali vya ujenzi pamoja na usimamizi wa usafi wa mazingira.
Msafara huo unaoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Mwl. Isihaka Rashid Mwalimu ambaye pia ni Mratibu wa Mapato wa manispaa ya Kibaha.
Lengo la ziara ni kuwajengea uwezo watendaji hao ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Katika ziara hiyo, watendaji hao watajifunza kutoka kwa wenzao wa Jiji la Mbeya juu ya mifumo na mikakati mbalimbali waliyoitekeleza kwa mafanikio katika ukusanyaji mapato, utoaji wa vibali vya ujenzi, na kuimarisha usafi wa mazingira.
Mwl. Rashid amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mikakati ya manispaa ya Kibaha kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kupitia ukusanyaji mzuri wa mapato na usimamizi bora wa mazingira.
Ziara hiyo inatarajiwa kuleta matokeo chanya yatakayosaidia Manispaa ya Kibaha kuongeza mapato ya ndani na kuimarisha huduma kwa wananchi wake.
Haki Zote Zimahifadhiwa