WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIBAHA WAMSHUKURU MKURUGENZI DKT. SHEMWELEKWA KWA SAFARI YA MAFUNZO
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha wamempongeza na kumshukuru Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Dkt. Rogers Shemwelekwa, kwa kuwapa motisha kupitia safari ya kikazi ya mafunzo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na mbuga ya wanyama ya Mikumi, mkoani Morogoro.
Pongezi hizo zimetolewa na Wakuu wa Divisheni na Vitengo walioshiriki katika ziara hiyo, ambapo baadhi yao walitembelea Mbuga ya Wanyama ya Mikumi kwa ajili ya kutalii na kuhamasisha utalii wa ndani, huku timu ya ukusanyaji mapato ikielekea Jiji la Arusha kwa ajili ya kujifunza mbinu mpya za ukusanyaji wa mapato na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa halmashauri hiyo.
Watumishi hao wameeleza kuwa safari hiyo ya mafunzo imekuwa chachu ya fikra mpya katika utendaji kazi wao wa kila siku. Wamesisitiza kuwa Dkt. Shemwelekwa ni kiongozi wa mfano anayejali ustawi na maendeleo ya watumishi wake, huku wakimhakikishia kuwa wataongeza bidii katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa kutumia mbinu walizojifunza.
Kwa pamoja, watumishi hao wamesema kuwa motisha hiyo imetoa hamasa kubwa ya kuongeza ubunifu na ufanisi katika utendaji kazi, hasa katika kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha huduma kwa wananchi wa Manispaa ya Kibaha.
Haki Zote Zimahifadhiwa