Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Zaidi ya wananchi 2500 huku 1611 waliovamia eneo la Mitamba kiwanja namba 34 wanatakiwa kuondoka kwenye eneo hilo iwapo watashindwa kulipia gharama nafuu za upangaji na upimaji kulingana na mahitaji ya Sasa.
Zoezi hilo linafanywa na Halmashauri ya Mji Kibaha yenye mamlaka kisheria baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuikabidhi eneo lenye Hekta 2963 lililoanza kuvamiwa na wananchi miaka 15 iliyopita na tayari kaya 1015 zimejengwa.
Kuondolewa kwao kumeibuliwa na kamati iliyoundwa na Wizara ya Ardhi ili kubaini ukweli wa nani ana haki ya kumiliki eneo hilo kati ya wananchi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi baada ya uwepo wa mkwamo wa Halmashauri Mji Kibaha kulipima kutoka kwa wananchi baada ya kukasimiwa na Serikali kama mamlaka ya upangaji kisheria
Hussein Sadick kando ya kuonesha vielelezo vyote vya umiliki halali Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwalipa fidia wananchi ili kulitwaa kihalali,wamewahoji wananchi 1611kati yao zaidi ya 1000 wamekiri kununua Viwanja kwenye kiwanja namba 34 kinyemela na wengine waliwasilisha nyaraka za mauziano feki zilizoandaliwa na matapeli wakiwemo viongozi wa Kuchaguliwa ngazi ya mitaa
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakar Kunenge amesema kipaumbele namba moja cha Serikali ya Mhe.Rais Samia ni kuwatumikia wananchi kwa kuheshimu haki na Utawala wa kisheria hivyo kwenye hili anayestahili haki atapewa na asiyestahili hatapona kwani watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria
Aidha,Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha imeagizwa kufuta michoro na Vibali vya ujenzi vilivyokwisha tolewa kwenye eneo hilo ili kuendelea na zoezi la upangaji na upimaji kwenye Mtaa mmoja uliosalia.
Awali wakati wa mikutano ya uhamasishaji na kutafuta suluhu ya eneo hilo,Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mheshimiwa Sara Msafiri aliwaambia wavamizi hao kuwa kujenga kwenye eneo lisilo lako kisheria ni sawa na kulala nje kwani muda usiotabirika mwenye nalo anaweza kulihitaji kwa matumizi mengine na kusababisha hasara kubwa kwenye familia,hivyo alitoa rai kwa wananchi kukubali kulipia gharama za kuhalalisha ukaazi wao kama zilivyowasilishwa na mamlaka ya upangaji,hata hivyo rai hiyo haikuwa na mafanikio.
Kwa Sasa Halmashauri ya Mji Kibaha inaendelea na upangaji na upimaji wa kiwanja namba 34 kwenye mitaa ya Lumumba,Kidimu na Mkombozi na baada ya kuhitimisha wavamizi hao watatakiwa kulipia shilingi 1,500 kwa kila mita ya Mraba ili kupata uhalali kwa kumiliki Ardhi kisheria
Haki Zote Zimahifadhiwa