TANGAZO KWA UMMA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI KIBAHA ANAWATANGAZIA WANANCHI NA WAWEKEZAJI WOTE KUWA HALMASHAURI IMEPIMA VIWANJA VYA MATUMIZI YA VIWANDA ENEO LA ZEGERENI, HIVYO ANAWAKARIBISHA KUNUNUA AU KUWEKEZA PAMOJA NA HALMASHAURI.
VIWANJA VINAUZWA KWA GHARAMA YA TSHS 8,000/= KWA MITA YA MRABA. WANANCHI,
MAKAMPUNI NA TAASISI ZINAZOHITAJI VIWANJA ZIFIKE OFISI YA MKURUGENZI WA MJI KIBAHA KUANZIA
TAREHE 8/ MEI, 2018 SIKU YA JUMANNE.
VIWANJA HIVI VIPO UMBALI WA KILOMITA NNE (4) KUTOKA VISIGA MADAFU BARABARA KUU IENDAYO MOROGORO KATIKA KATA YA MISUGUSUGU MTAA WA ZOGOWALE.
HUDUMA YA UMEME NA MAJI ZIPO ENEO LA MRADI NA BARABARA ZINAPITIKA WAKATI WOTE WA MWAKA NA PIA KUNA BAADHI YA VIWANDA VIMEANZA KUFANYAKAZI KAMA VILE VIWANDA VYA NONDO, GYPSUM, KUKOBOA NA KUSINDIKA
NAFAKA NK.
MWOMBAJI ANATAKIWA KULIPA TSHS. 20,000/= ADA YA MAOMBI AMBAYO HAITARUDISHWA.
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISI YA MKURUGENZI WA MJI.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI WA MJI
HALMASHAURI YA MJI KIBAHA
Haki Zote Zimahifadhiwa