Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Jumla ya Watahiniwa 5587 wa darasa la Saba wa Halmashauri ya Mji Kibaha leo Septemba 13,2023 wameketi kuanza duru ya awali ya mtihani wa kutamatisha masomo ya Elimu ya Msingi,safari waliyoanza Mwaka 2017.
Adinan Livamba,Afisa Elimu taaluma amesema kati ya Watahiniwa hao wavulana ni 2705 sawa na asilimia 48.4, wasichana wakiwa 2882 sawa na asilimia 51.6 ambapo jumla ya mikondo 249 inatumika
Aidha,Livamba amesema kuwa katika mtihani huo wapo wanafunzi wenye ulemavu 18 kati yake 12 ni wanaume na Wanawake ni 6 walioandaliwa mikondo 8 ambapo Wanaume watakuwa na mikondo 5 na Wanawake mikondo 3.
Afisa Elimu Kata ya Pangani Juma Karuja amesema kwa ujumla watahiniwa wote wameandaliwa vizuri kuliko wakati mwingine hivyo matarajio yao watafaulu kwa ufaulu mzuri
Tathmini ya ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo kati ya Mwaka 2020-2022 inaonesha wastani wa ufaulu kuwa ni asilimia 94.6 hivyo matarajio yetu kwa mwaka huu 2023 ni 98
Baraza la Madiwani,Menejimenti na watumishi wote wa Halmashauri ya Mji Kibaha wanawatakia kila la kheri.
Haki Zote Zimahifadhiwa