Na Byarugaba Innocent, Morogoro.
Maelfu ya wahudhuriaji wamefurahishwa na Banda la Halmashauri ya Mji Kibaha kwenye Maonesho ya 29 ya nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Mkoani Morogoro.
Maonesho ya nanenane Mwaka huu yamebabe kauli mbiu isemayo;agenda 10/30 Kilimo ni biashara;jiandae kuhesabiwa kwa Mipango bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi ambapo kwa Kanda ya Mashariki inayohusisha Mikoa ya Dar-es-Salaam, Pwani, Tanga na mwenyeji Morogoro
Aidha,baada ya Agosti 6,2022 kutembelewa na Wakulima na Maafisa ugani toka Kibaha Mji,leo Agosti 7 Wakuu wa Idara na vitengo wamefika kujionea Maendeleo ya Maonesho yanayoendelea ambapo wameridhishwa na mwenendo chanya waliouona ilhali maandalizi yalikuwa ya muda muda mfupi.
Waliofika leo ni Afisa Utumishi na Utawala Protas Dibogo,Mwanasheria Mansuetha Mbena,Afisa TEHAMA Fred Mwanyelele,Optuna Kasanda na Afisa Usafishaji Mazingira Ally Hatibu aliyekuja na familia yake.
Aidha,mara baada ya kufika walipokelewa na kupewa Elimu ya kuotesha mbogamboga na mwenyeji wao Afisa Kilimo Joseph Njau na kuonesha kuvutiwa na aina hiyo ya Kilimo kwani kando ya kuwa na eneo dogo unaweza kuzalisha na kupata mavuno ya kutosha.
Baada ya hapo kingine kwenye Banda hilo imekuwa ni Ufugaji wa Samaki ambapo Afisa Samaki Elias Kasema aliwaeleza kuwa ukitaka kufuga kwa tija zaidi wafuge Samaki dume kauli iliyoaawacha midomo wazi kuwa hata Samaki wanajinsia kama walivyo wanyama na Ndege.
"Binafsi leo nimejifunza kitu,sikujua kama unaweza kuwatambua Samaki jike na dume,alisema Dibogo"
Kasema aliongeza kuwa njia rahisi ya kutambua jinsia zao ni rahisi kwani umbo kubwa na uzuri wa rangi ni kiashiria mojawapo cha kuwatambua.
Maeneo mengine waliyotembelea ni ufugaji wa Ng'ombe, Kuku,Kanga,Bata na Bata Mzinga.
Njau na Afisa Mifugo wa Halmashauri ambao ni waandaji Wakuu wa Maonesho haya kwenye halmashauri wametoa rai kwa wananchi hususan wa Kibaha Mjini kufika Kwa wingi kujifunza hasa Kilimo na Ufugaji Mijini kwani unaweza kuwa sehemu ya kukuza vipato katika familia
Maonesho haya yalifunguliwa Agosti 4,2022 na Waziri Mkuu mtaafu Mhe.Mizengo Kayanza Peter Pinda na yanatarajiwa kufungwa kesho Jumatatu Agosti 8,2022 na Makamu wa pili wa Serikali ya Mapinduzi -Zanzibar
Haki Zote Zimahifadhiwa