Na Byarugaba Innocent
Wawekezaji na wafanyabiashara wameaswa kuwa wazalendo kwa kulipa Kodi na kuwasilisha taarifa sahihi za biashara zao ili kuiwezesha Wilaya kupata Mapato yatakayotumika kujenga miundombinu na Maendeleo mengine Kisekta
Rai hiyo ilitolewa Muhammad Tundia ambaye ni Mwenyekiti za Baraza hilo Wilaya kwenye mkutano wa baraza lililoketi Januari 19,2023 kwenye Ukumbi wa Njuweni Kibaha kujadili changamoto na fursa za uwekezaji.
Aidha,Tundia alitoa ombi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Sarah Msafiri kuitisha vikao vya mara kwa mara Kisekta vitakavyotoa mwanya kwa wawekezaji na wafanyabiashara kuwasilisha kero wanazokumbana nazo.
Akiwasilisha fursa za uwekezaji Afisa biashara wa Halmashauri ya Mji Kibaha Adolf Msangi alisema maeneo makubwa yametengwa kwa ajili ya uwekezaji mkubwa na mdogo kwenye sekta za Michezo,Usafirishaji,Makazi,Kilimo,Elimu na huduma za afya na kutoa rai kwa wawekezaji kuwekeza huku ahadi ya Halmashauri ni kutoa ushirikiano kufanikisha uwekezaji huo.
Aidha,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde akipokea maelekezo ya maboresho yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu ya kuvutia zaidi kwenye Maeneo hayo ili kuwavuta wawekezaji.
Mkutano huo kadhalika ulihudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Biashara nchini Dkt.Godwilly Wanga aliyeahidi kwenda kushughulikia suala la ulinganifu wa Mapato kati ya Mkoa wa Pwani na Dar-es-Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kodi (TRA) ili kuleta usawa tofauti na Sasa ambapo wawekezaji wa viwanda wengi wapo Pwani lkn Mapato wanalipia Dar-es-Salaam wanakouzia na kufanya Mapato kuwa kidogo Mkoa wa Pwani.
Haki Zote Zimahifadhiwa