Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha kiasi cha Bilioni 1.3 kwa Halmashauri ya Mji Kibaha kwa ajili ya upanuzi wa hospitali ya Wilaya Lulanzi.
Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri Dr.Tulitweni Mwinuka imeonyesha kuwa kiasi cha fedha milioni 500 kilipokelewa Oktoba 27,2021 huku awamu ya pili kikipokelewa Mei 27,2022 kwa ajili ya Ujenzi wa wodi tatu,jengo la upasuaji na chumba cha kuhifadhia maiti.
Mhandisi wa Halmashauri ya Mji Kibaha John Alexander ameeleza kazi zinazoendelea kuwa ni upasuaji na upigaji rangi hatua ya awali kwenye wodi ya watoto iliyofikia asilimia 67 huku wodi ya Wanaume na wanawake ikifikia 77 asilimia.Aidha,jengo la upasuaji na chumba cha maiti imefikia hatua ya upandishaji wa tofali.
Mkurugenzi wa Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya na kwamba fedha hiyo atahakikisha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwa na Majengo imara yatakayo wanufaisha wagonjwa 100,000-200,000 kwa Mwaka.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mussa Ndomba ametoa rai wataalam kuitunza miundombinu hiyo huku wakitekeleza majukumu yao ya Msingi ya kutoa huduma kwa kuzingatia weledi,sheria,Kanuni, taratibu,miongozo yote kutokana na viapo vyao ili kuendelea kumheshimisha Mama Samia anayejali afya za Wananchi wake.
Haki Zote Zimahifadhiwa