Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mheshimiwa Nickson Simon amefanya ziara kukagua Maendeleo katika sekta ya Elimu kwenye shule ya Sekondari Mwambisi na kuweka mkakati kabambe wa kuongeza ufaulu na kufuta daraja sifuri.
Awali Mkuu wa shule hiyo Joseph Simba alieleza kuwa mpango wao wa ndani kuongeza ufaulu kufikia asilimia 50 kwa daraja A-C huku asilimia 50 nyingine ikifuta daraja sifuri na tayari utekelezaji umeanza.
Akiongea na walimu 49 kati ya 54 wa shule hiyo kwa niaba ya Walimu 820 wa Halmashauri ya Mji Kibaha,Mheshimiwa Simon amesema kazi ya ualimu ni mwanzo wa taaluma nyingine hivyo inabidi kutekelezwa kwa juhudi,maarifa,weledi na Upendo mkubwa hasa kwenye Mazingira haya ambayo baadhi ya wazazi wametekeleza majukumu yao.
"Wazazi hawanunui vitabu,hawawapangii watoto wao ratiba za kujisomea,wala hawaweki malengo ya kitaaluma kwa watoto wao,mzigo wote wameacha kwa walimu" amesema DC na kutoa rai kwa walimu kuongeza ubunifu ambao mara zote hauna mipaka.
Mheshimiwa Simon ametoa ushauri kwa walimu wote kuwa na ubao wataoorodhesha vipaumbele vya kitaaluma vinavyowasumbua na kila watakapokuwa watavitafutia ufumbuzi itakuwa na utekelezaji wa mkakati wa kuwaokoa wanafunzi na ziro.
Mkuu wa Wilaya ameahidi kutoa motisha ya Viwanja vya makazi kwa walimu wataofanya vizuri na kufikia malengo ya Kiwilaya.
Katika Mtihani wa kuhitimu kidato cha nne Mwaka 2022 kati ya wanafunzi 192 walifanya mtihani ni wanafunzi 17 pekee walifaulu kwa daraja la 1-3 huku wanafunzi 175 wakiambulia daraja 4 na sifuri hivyo kuifanya shule kuwa nafasi ya 19 kati ya 19 ya shule za Serikali Kibaha Mjini.
Haki Zote Zimahifadhiwa