Dkt. Rogers Shemwelekwa Ashiriki Maonesho ya Wakulima Morogoro, Atoa Wito kwa Wakulima na WafugajiMkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, akiwa ameambatana na Wakuu wa Divisheni na Vitengo kutoka Halmashauri hiyo, ameshiriki kikamilifu katika maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Mkoa wa Morogoro.
Akiwa katika Banda la Manipaa ya Kibaha Dkt. Shemwelekwa amekona teknolojia bunifu za kilimo cha kisasa, hususan teknolojia za kilimo cha wavu pamoja na mifugo, amepongeza maendeleo ya kilimo na mifugo katika kuhakikisha wakulima na wafugaji wanapata elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya teknolojia katika kuongeza tija na ubora wa mazao yao.
Dkt. Shemwelekwa ametoa wito kwa wakulima na wafugaji kote nchini, hususan wa Manispaa ya Kibaha, kutumia teknolojia hizo katika shughuli zao ili kuongeza uzalishaji na kuinua kipato chao. Amehimiza wakulima wa maeneo ya mijini kutumia fursa ya kilimo cha mjini, kwa kuzingatia ufinyu wa ardhi na mahitaji ya soko la bidhaa za kilimo ndani ya miji.
“Kilimo cha mjini kina faida kubwa si tu kwa kipato bali pia kwa usalama wa chakula kwa kaya. Ni wakati sasa wa wakazi wa Manispaa ya Kibaha kuchangamkia fursa hizi kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira na zenye tija,” alisisitiza Dkt. Shemwelekwa.
Maonesho ya Nanenane ni jukwaa muhimu linalowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo na mifugo, na mwaka huu yameendelea kuonyesha ubunifu na teknolojia mpya zinazolenga kuongeza ufanisi katika sekta hizo
Haki Zote Zimahifadhiwa