Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon mapema leo ameongoza kikao cha tathmini ya Mkataba wa lishe ngazi ya Kata ambapo hali imeonesha kupanda kwa asilimia 20 kutoka 60 robo iliyopita mpaka 80 kwa robo ya nne ya Mwaka 2022/2023
Mtendaji wa Kata ya Sofu Saumu Nkulo ameeleza kuwa siri ya Mafanikio ni kufanya hamasa,kuandaa vikao vya Wazazi vyenye agenda ya lishe na ushirikishwaji wa wazazi kwenye kupanga mikakati ya lishe kwa watoto shuleni ili kuimarisha afya zao wakati wa masomo.
Aidha,mtendaji wa Kata ya Misugusugu Elizabeth Mwakaliku amekiri baadhi ya changamoto ya uhamasishaji lishe hivyo ameomba uwepo wa ushirikiano kati ya Watendaji,wazazi na wadau wengine wa Maendeleo ili kuweza kufikia malengo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde ametoa rai kwa wazazi na walezi kushiriki kikamilifu kuchangia lishe kwa watoto wao ili kuimarisha afya za watoto na kufikia lengo la Serikali
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon ametoa rai Watendaji wa Kata kuongeza kasi ya ufuatiliaji na wabunifu kwenye kutoa hamasa,kupanga vikao kulingana na uhitaji na kuwatumia wazazi wenye mwitikio wa kushiriki kuwa wazungumzaji kwenye vikao sambamba na kujifanyia tathmini kulingana na utekelezaji wao
"...msifanye vikao kwa kufuata ratiba,fanyeni vikao kulingana na uhitaji kwani suala hili tumesaini Mkataba na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,tunapaswa kulitekeleza kwa Mafanikio makubwa "amesema Mhe.Simon
Mratibu wa lishe wa Halmashauri ya Mji Kibaha Salma Mohamed amewasihi Watendaji wa Kata kuongeza ya utekelezaji ili kuendelea kuboresha hali za lishe shuleni.
Haki Zote Zimahifadhiwa