Morogoro, Agosti 2, 2025 – Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha inashiriki kikamilifu katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane, Manispaa ya Morogoro.
Kupitia banda lake, Manispaa ya Kibaha inaonesha ubunifu na teknolojia mbalimbali zinazolenga kuhamasisha maendeleo ya kilimo na ufugaji kwa wananchi pamoja na bidhaa mbalimbali za wajasiriamali . Miongoni mwa teknolojia zinazopatikana katika banda hilo ni ufugaji wa kisasa wa kuku, samaki, kanga, na bata, pamoja na mbinu bora za uzaliwhaji wa malisho ya mifugo.
Aidha, wananchi wanaopata fursa ya kutembelea banda hilo wanapewa elimu ya lishe, huduma ya upimaji wa virusi vya UKIMWI (VVU), pamoja na mafunzo ya kilimo cha mbogamboga chenye tija kwa kutumia teknolojia rahisi na rafiki kwa mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa maafisa kutoka Manispaa hiyo alieleza kuwa ushiriki wao katika maonesho hayo ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha elimu ya kilimo na ufugaji inawafikia wananchi kwa njia ya vitendo.
“Tunawaalika wananchi wote kutembelea banda la Manispaa ya Kibaha ili kujionea bunifu zetu na kujifunza mbinu bora zitakazosaidia kuinua maisha yao kupitia sekta ya kilimo na ufugaji,” alisema afisa huyo.
Karibu Banda la Nanenane Manispaa ya Kibaha – Ujionee, Ujifunze na Uboreshe Maisha Yako!
Haki Zote Zimahifadhiwa