Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Jumla fedha kiasi cha shilingi 8,135,943,122.03 zimetumika kutoa huduma za maendeleo kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde ameeleza kuwa fedha hizo zipo katika makundi manne ambayo ni fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha shilingi 1,969,958,103.91,fedha za nje zinazotoka kwa wahisani na wadau wa Maendeleo shilingi 2,506,280,585,fedha zilizopokelewa nje ya bajeti shilingi 2,217,688,000 na fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri shilingi 1,442,016,433.12
Aidha,Munde amesema fedha hizo zimetumika kununua samani, kujenga miundombinu na kuboresha huduma za Elimu,afya,kutoa Mafunzo na kuimarisha afya za wananchi pamoja na kuimarisha vyanzo vya Mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kuridhia fedha hizo zitumike kwa ajili ya wananchi na kwamba huo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.
Aidha,Ndomba amewashukuru washirika wa Maendeleo kwa kuchangia pamoja na Wananchi kuendelea kulipa Kodi zinazowezesha utoaji wa huduma kwenye Mji wa Kibaha.
Mhe.Ndomba ametoa rai kwa wataalam wa Halmashauri kutumia taaluma zao ili kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa weledi na thamani fedha inayotumika iendane na thamani mradi husika.
"...Wananchi kazi yenu ni moja tu,miradi hii inayotumia gharama kubwa kuijenga,lindeni ili itumike muda mrefu na vizazi vijavyo..'amesema Ndomba.
Haki Zote Zimahifadhiwa