• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

IMARISHENI UTENDAJI KAZI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU- NDUNGURU

Posted on: June 29th, 2023

Na. Asila Twaha, Morogoro

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Adolf Ndunguru amewataka  Wasimamizi wa Elimu kwenye  Sekretarieti  za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuimarisha utendaji kazi wao ili kufikia matokeo chanya ya kuboresha elimu yaliyokusudiwa na Serikali katika  ngazi zote za elimu.

Ndunguru ameyasema hayo Juni 28, 2023 wakati akifunga  mafunzo ya  Matumizi ya Njia na Vifaa vya Mtaala wa Elimu ya Awali vilivyoboreshwa kwa Walimu wa Elimu ya Awali yaliyofanyika  katika chuo cha Ualimu Mkoani Morogoro.

Amesema kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) kwa mwaka 2022/23 Serikali imetoa jumla ya Shilingi bili. 230 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za msingi 302 zenye vyumba vya madarasa vya mfano vya elimu ya awali, vyumba vya madarasa 2,929, madarasa ya awali ya mfano 368 yanajengwa kwenye shule zilizopo.

“Miundombinu hii itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani, umbali wanaotembea wanafunzi kwenda shule, vikwazo vya usalama wa wanafunzi kufika shule”  amesema Ndunguru

Ameongezea kusema, Serikali imeendelea kuajiri walimu ili kuhakikisha kila mwanafunzi anajifunza kwa ufanisi kwa mwaka 2019/20 hadi 2022/23 jumla ya walimu 55,601 waliajiriwa, wakiwemo 2,304 wa elimu ya awali, 29,904 wa elimu ya msingi, na 23,393 wa elimu ya sekondari.

 Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuyatumia vyema ikiwemo mada walizofundishwa, mbinu ya kutengeneza zana zinazoendana na mazingira yanayomzunguka mtoto, mbinu shirikishi za kuwezesha ufundishaji kwenye madarasa jumuishi, njia za kushirikisha jamii katika kutoa huduma kwa watoto wa elimu ya awali, miongozo iliyoboreshwa ya ujifunzaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na stadi za malezi yenye mwelekeo chanya.

Aidha, amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha mafunzo ya walimu wanaofundisha elimu ya awali yanaendeshwa kwa ukamilifu na ufanisi kwenye vituo vyote 22 vilivyochaguliwa kama ilivyopangwa.

Ametoa wito kwa Viongozi wa Elimu kuhakikisha walimu wote wanaopatiwa mafunzo wanaporudi vituoni waendelee kupangiwa kufundisha madarasa ya elimu ya awali ili ujuzi wao uendelee kutumika na lengo la kuboresha ujifunzaji wa mwanafunzi wa elimu ya awali lifikiwe.

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimumsingi  na Awali TAMISEMI Bi. Susana Nussu amesema, mafunzo yatahusisha washiriki 4,240 wakiwemo wawezeshaji wa kitaifa 110, walimu wanaofundisha elimu ya awali 3000, walimu wakuu 552 na maafisa elimu kata 552.

Amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa afua ya Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi(BOOST).

Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN KIBAHA TOWN UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • TANGAZO LA MNADA WA NG'OMBE KWA WAFANYA BIASHARA WA NYAMA NA NG'OMBE ,MTAA WA MTAKUJA KATA YA PANGANI, UNAOFANYIKA KILA ALHAMISI. March 13, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • ZOEZI LA MABORESHO YA DAFTARI LA WAPIGA KURA KUANZA MEI 16 KIBAHA TC

    May 09, 2025
  • KIBAHA MANISPAA YANG'ARA UKUSANYAJI WA MAPATO

    April 30, 2025
  • DKT.SHEMWELEKWA ATETA NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KIBAHA Na.Byarugaba Innocent, Kibaha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufa

    November 22, 2024
  • DKT.SHEMWELEKWA ATETA NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA KIBAHA Na.Byarugaba Innocent, Kibaha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufa

    November 22, 2024
  • Tazama Zote

Video

Mh. Waziri Mkuu akiwa ziarani Kibaha
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa