Na Byarugaba Innocent,Morogoro.
Wananchi wameaswa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutembelea vivutio vya Utalii hasa wa ndani ili kuzifahamu rasilimali zao pamoja na kuongeza Mapato ambayo yamekuwa yakitumika kutolea huduma kwa wananchi wenyewe nchini.
Hayo yameelezwa na Tatu Mwambala Mkuu wa shule ya Sekondari Zogowale ambaye ameambatana na walimu wake 30 kutembelea hifadhi ya Taifa Mikumi iliyopo Mkoa wa Morogoro kama sehemu ya kuwapa motisha walimu kwa kufanikisha ufaulu mzuri wa Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita,2022
Mwambala amesema kuwa kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo ni kuunga mkono juhudi za Rais wetu kwani pamoja na Majukumu mengi aliyonayo ya kuliongoza Taifa,bado alitenga muda wa kucheza filamu ya "Tanzania the royal tour"ambayo imefungua fursa zaidi za Utalii kwa mataifa mengine kwa kuonesha rasilimali nyingi zilizopo na Sasa watalii wameongezeka nchini tafauti na miaka ya nyuma
"Kama unavyojionea mwenyewe mwandishi,mimi nimekuja hapa kutalii mara nyingi,lakini tangu filamu ya mama imeoneshwa,Tanzania imefunguka zaidi,imepanua wigo wa wahudhuriaji na Sasa wanafika wengi,tazama umati huu"..amesema Mwambala
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa shule hiyo Laurent Valentine Ntwale amesema ni wakati muafaka kwa walimu kutembelea vivutio vya Utalii hasa wakati wa likizo ili kuongeza Mapato ambayo yamekuwa yakitumika kuboresha na kuongeza miundombinu ya Elimu mathalan vyumba vya Madarasa ili kupunguza mlundikano wa wanafunzi darasani,Mabweni,nyumba za walimu,samani na kwamba maboresho haya huongeza juhudi na hamasa Ari ya kufundisha kwa walimu na kupelekea ufaulu wenye tija.
Calvin Mmari,Mwalimu wa taaluma shuleni hapo amesema kando ya kufanya ziara ya hiyo kwa lengo la kujifunza na kuwamotisha walimu amesema huo ni utaratibu ambao wamejipangia kama sehemu ya kuunga jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwafadhili wanafunzi wa kike wanaodahiliwa kusoma masomo ya Sayansi ili kuja kulitumikia Taifa
Hii ni mara ya tatu kwa walimu wa shule ya Sekondari Zogowale kufanya Utalii wa ndani.Awali Mwaka 2020 walikwenda hifadhi ya Saadani,Mwaka 2021 wakaenda Kaole Bagamoyo na 2022,wamefika hifadhi ya Mikumi.
Haki Zote Zimahifadhiwa