Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Katika kuadhimisha siku ya kichaa Cha Mbwa duniani kila Septemba 28,Halmashauri ya Mji Kibaha leo Septemba 2022 imeanza zoezi la kuchanja Mbwa na Paka 500 bure kama sehemu ya kutoa Elimu pamoja na kuhamasisha Jamii Kuhusiana na Ugonjwa wa Kichaa Cha Mbwa.
Aidha,zoezi hili katika Mipango ya Halmashauri litahitimishwa tarehe 2 Oktoba,2022 ili kutoa fursa kwa wananchi wote kufanikisha uchanjaji kwa Mifugo hiyo kwenye vituo vya Kata za Kibaha , Mailimoja , Tumbi , Mkuza , Sofu Pangani
Dkt.Deogratius Mgute ameeleza kuwa kwa Mwaka huu wa fedha Halmashauri inatarajia kununua dozi 100 zenye thamani ya Shilingi 1,500,000.00 za Mapato ya ndani zitakazowezesha kuchanja Mbwa na Paka 1000 ili kukabiliana na ugonjwa hatari wa kichaa cha Mbwa kando na 500 wanaogharamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Aidha,Dkt Mgute ametoa rai kwa wananchi ambao hawatafikiwa na zoezi hili kwa Sasa kuhamasika kununua chanjo na Halmashauri itatoa wataalam wa kwenda kuwachanja ili kuepusha madhara ya kichaa cha Mbwa vikiwemo vifo.
Hata hivyo watalaam wa Afya wanasema pamoja na kuwa kichaa cha Mbwa Kinaua,bado kinaweza kuzuilika kwa kuwachanja Mbwa na Paka kila Mwaka,kuepuka kuwa katika Mazingira ya kung'atwa,kuosha jeraha kwa sabuni na Maji mengi yanayotiririka kwa dakika 15 na kutofunga kidonda kabla ya kwenda Kituo cha Afya kwa matibabu zaidi.
Takwimu za madhara makubwa zinaonesha kuwa kila dakika moja,mtu mmoja hufariki Dunia ambapo watu 59,000 Dunia hufariki kila Mwaka.Aidha,barani Afrika watu 21,476 hufariki kila Mwaka huku Tanzania watu 1500 wakipoteza maisha kila Mwaka kwa kichaa cha Mbwa
Halmashauri ya Mji Kibaha yenye Mitaa 73 na Kata 14 inakadiriwa kuwa na Mbwa 3114 na Paka 930.
Kauli mbiu ya siku ya Kichaa cha Mbwa Mwaka,2022 ni;Afya yako,bila kifo.
Haki Zote Zimahifadhiwa