Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Jumla ya bajeti ya Shilingi bilioni 48,655,452,236 imepitishwa na Baraza la Madiwani la Kibaha Mji lililoketi leo Jumatano 22,2023 kuridhia na kupitisha makadirio na Matumizi kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa na ongezeko la bilioni 2,845,940,730 ukilinganisha na bajeti ya Shilingi 45,809,511,506 ya Mwaka wa fedha 2022/2023.
Mhe.Kambi Legeza Diwani wa Kata ya Visiga aliyewasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti Mhe.Selina Msenga amesema kati ya fedha hizo,Shilingi bilioni 6,563,628,000 ni Mapato ya ndani,Bilioni 41,161,858,000 ni ruzuku kutoka Serikali kuu na wafadhili mbalimbali huku Milioni 929,966,236 zikitoka kwenye vyanzo vingine ikiwemo Bima ya afya na Mchango wa Jamii.
Akifafanua matumizi ya fedha hizo Mhe.Legeza ameeleza kuwa jumla ya fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 31,094,816,000 itatumika kulipa mishahara ya watumishi,milioni 824,226,000 ikitumika kwa matumizi ya kawaida na Miradi ya Maendeleo ikitumia kiasi cha Bilioni 9,242,816,000
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba amesema kuwa bajeti ya Mwaka 2023/2024 imekuwa shirikishi kwani imeanza kuchakatwa kuanzia ngazi ya Mtaa na itatekeleza vipaumbele vya Wananchi ikiwemo Elimu,Afya,Maendeleo ya Jamii kwa kutoa Mikopo ya akina Mama,Vijana na wenye ulemavu.Aidha,ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji ili kufikia malengo.
wenyekiti umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mji Ramadhani Kazembe amewapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa kazi nzuri wanayoendelea kujifanya na kwamba uzuri wa bajeti hiyo inakwenda kuitekeleza ilani cha CCM kwa vitendo.
Bajeti imepitishwa na Waheshimiwa Madiwani wote kwa asilimia mia moja.
Haki Zote Zimahifadhiwa