MAAFISA WA TAKUKURU WATOA ELIMU YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI KIBAHA
Maafisa wa TAKUKURU wametembelea Watumishi wa Halmashauri ya Mji Kibaha kwa lengo la kutoa Elimu kuhusu mbinu za kuzuia na kupambana na Rushwa, hasa katika ukusanyaji wa Mapato. Katika semina hiyo, walijadili njia mbalimbali za kuhakikisha kuwa mapato ya Halmashauri yanakusanywa kwa njia za kisheria na zinazoheshimu maadili ya Utumishi wa Umma. Walisisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika michakato yote ya ukusanyaji wa Mapato ili kuepuka mianya ya Rushwa na upotevu wa Fedha za Umma.
Aidha, walieleza umuhimu wa kuweka mifumo madhubuti inayoweza kufuatilia na kudhibiti Mapato kwa usahihi na ufanisi. Kwa kufanya hivyo, walitarajia kuongeza Uaminifu na Uadilifu miongoni mwa watumishi wa Halmashauri na kuboresha huduma kwa wananchi.
Maafisa Kutoka TAKUKURU walitoa pongezi kwa Halmashauri ya Mji Kibaha kwa juhudi zao za ukusanyaji mzuri wa mapato, hatua ambayo inachangia katika maendeleo ya Mji huo.
Elimu hii inalenga kuhakikisha kuwa watumishi wanakuwa na uelewa mzuri kuhusu athari za rushwa na umuhimu wa kuzingatia maadili katika utendaji kazi wa kila siku
Haki Zote Zimahifadhiwa