HALMASHAURI ya Manispaa ya Kibaha imefanya Uzinduzi wa Wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama duniani, uliofanyika katika Zahanati ya Mwendapole Kata ya Kibaha.
Akiongea na wananchi na wananchi kwenye uzinduzi huo Afisa lishe Neema Bernad aliyemwakilisha Mganga mkuu wa Manispaa ya Kibaha ameelezea faida za kunyonyesha maziwa ya mama Kwa mtoto , na kusisitiza kwamba mwanzo Bora wa mtoto huanza Kwa kunyonyesha maziwa ya mama ambayo yanamjengea Kinga dhidi ya maradhi mbalimbali na kuondokana na tatizo la udumavu Kwa watoto.
Wananchi walishukuru kupata elimu ya unyonyeshaji na kuomba iwe endelevu.
Elimu ya unyonyeshaji inaendelea kutolewa Kwa wiki nzima ya maadhimisho.
Haki Zote Zimahifadhiwa