Na.Byarugaba Innocent, Morogoro
Jana Agosti 8,2022 Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Sera, Bunge na uratibu Mhe.George Simbachawene (MB) amehitimisha Maonesho ya 29 ya nanenane kanda ya Mashariki yaliyoanza Julai 31kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Morogoro
Aidha, Maonesho kanda ya Mashariki inayohusisha Mikoa ya Dar-es-Salaam Pwani Morogoro na Tanga yalizinduliwa Agosti 4,2022 na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Peter Pinda yakiwa na washiriki zaidi ya 400
Mheshimiwa Simbachawene amekiri kuridhishwa na maandalizi pamoja na maonesho yenyewe na kutumia fursa hiyo kuwapongeza waandaji kwa kushirikiana vema kufanikisha Maonesho hayo ambayo ni nyenzo muhimu kwa wadau wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kubuni ujuzi na teknolojia mpya ili kuongeza uzalishaji,usindikaji kwa tija na Uhifadhi wa mazao.
Ameongeza kuwa Mchango mkubwa wa sekta hizi umekuwa ukionekana kwenye kuchangia Pato la Taifa,usalama wa Chakula na malighafi viwandani hivyo ametoa rai kwa wananchi kushiriki kuhesabiwa wakati wa sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23,2022 nchini ili kuiwezesha Serikali kupanga Mipango Bora na endelevu kwenye sekta hizo za Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi,Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anton Mavunde (MB) ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa Kilimo na kuongeza bajeti ya Wizara kutoka Bilioni 200 mpaka kufikia Bilioni 900 ambapo tayari fedha hizo mishapangiwa Mipango thabiti na Wizara ili kuinua sekta hizi ikiwemo kununua vyombo vya usafiri mathalani Magari na Pikipiki zitakazotolewa kwa maafisa ugani nchini ili kuwafikia wakulima.Aidha,Ndege kwa ajili ya kunyunyizia dawa za kuua wadudu waharibifu mashambani itanunuliwa katika mipango iliyopo
Akihitimisha Maonesho ya 29 ya nanenane Kitaifa Kanda ya Nyanda za juu kusini yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya John Mwakangale,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wakulima wote kujisaji kwenye kanzidata maalum ili Serikali iwatambue
"Niombe wakulima wote nendeni kujisajili,mbele huko tutatoa vitambulisho kwa wakulima,kitambulisho chako kitakufanya ukapate huduma kadhaa ikiwa mkopo,ikiwa ruzuku,ikiwa mambo mengine ...sasa ukifanya uzembe kwenda kujisajili,utakapo kwenda kupata huduma huna kitambulisho hasara itakuwa kwako"alisema Rais Samia
Maonesho 29 ya nanenane Mwaka 2022 yamekuwa na Kauli mbiu isemayo; Agenda 10/30 Kilimo ni biashara;Shiriki kuhesabiwa kwa Mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Haki Zote Zimahifadhiwa