• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MHE.MCHENGERWA ATEMA CHECHE KWENYE UTIAJI SAINI WA MIKATABA YA REGROW YA BILLION 157

Posted on: April 17th, 2023

Mhe. Mchengerwa atema cheche kwenye utiaji saini wa  mikataba ya REGROW ya bilioni 157, asisitiza REGROW utafungua utalii na uchumi wa mikoa ya kusini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa  amewataka  watekelezaji wote  wa Mradi  wa Kuboresha  Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii kusini (REGROW) kuondoa ukiritimba   wakati wa kutekeleza  mradi  huu ili  kukuza  na kutangaza mazao mapya  ya utalii katika mikoa ya  kusini mwa Tanzania vinginevyo  hatua  kali zitachukuliwa  kwa watakaobainika  kufanya  uzembe au kuuhujumu mradi huo.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo  leo Aprili 16, 2023 jijini Arusha wakati  akitoa  hotuba yake kwenye hafla ya utiaji saini mikataba nane  ya ujenzi wa miundombinu  yenye thamani ya shilingi  bilioni 157.29 chini ya mradi wa  kuboresha  usimamizi  wa Maliasili  na  kukuza utalii kusini mwa Tanzania.

“Wanaopaswa kwenda kusimamia  lazima waende wakasimamie na watendaji ambao  watabainika  kutofanya  vizuri watachukuliwa hatua, dhamira ya serikali ni kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri ili twende  tukapate fedha zaidi  katika  awamu ya pili.” Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Waziri Mchengerwa amewataka  wakandarasi wote waliosaini mikataba hiyo kutumia vizuri muda waliopewa kwa kufanya kazi nzuri katika muda mfupi na kwamba wasitarajie kuongezewa  muda.

Mikataba  iliyosainiwa imegawanyika katika makundi mawili; mikataba minne ya ujenzi wa majengo pamoja na mikataba minne ya ujenzi wa viwanja vya ndege ambayo itatekelezwa katika hifadhi  nne za Ruaha, Mikumi Udzungwa na Nyerere na Msitu wa Asili wa Kilombero chini ya TFS 

Akifafanua  zaidi amesema kwenye  mikataba ya ujenzi wa viwanja inatarajiwa  viwanja sita  vya ndege kujengwa ambapo viwanja vitatu vya ndege vitajengwa hifadhi ya  Ruaha  , viwanja viwili  hifadhi ya Mikumi  na hifadhi ya Nyerere  kitajengwa kiwanja  kimoja cha ndege.Aidha amesema katika hifadhi ya Udzungwa  kutajengwa njia ya juu ya watalii ambayo inakadiriwa kuwa na kilomita moja ambayo inatarajiwa kuwa  miongoni mwa njia   ndefu zaidi Afrika Mashariki na hata kusini mwa Afrika itakapokamilika.

 Mhe. Mchengerwa amefafanua  kuwa miundombinu  mbalimbali kama vile majengo ya utalii, mageti, vituo vya habari, nyumba za watalii, hosteli vituo vya askari pamoja  na maeneo ya kupumzikia yatajengwa  ili kuhakikisha watalii wanafurahia wanapotembelea katika maeneo hayo.

Amesema ujenzi wa miradi hii itasaidia kufungua fursa na kukua kwa uchumi wa mikoa ya kusini na amewaomba wakazi wa mikoa ya kusini kuchangamkia  fursa  wakati wa utekelezaji wa miradi.

Aidha, Mhe.Mchengerwa ametoa wito kwa  wananchi wa  Mikoa ya Kusini kuchangamkia fursa za ajira zitakazotokana na utekelezaji wa mikataba hiyo ambapo amewasisitiza  watakaopata kazi hizo   wakawe wazalendo na  wafanye kazi kwa bidii ili kwa pamoja mradi huo uweze kuchagiza  maendeleo ya  ukuaji wa Sekta ya Utalii pamoja na kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja.

Katibu Mkuu wa  Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi ameelezea  kusikitishwa kwake  kwa jinsi ambavyo mradi umekuwa ukishindwa kutekelezwa bila sababu zozote za msingi ambapo hadi Machi mwaka huu mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 43 tu na kuonya kuwa hatamfumbia macho mtekelezaji yoyote wa mradi huo.

Mradi  REGROW ulianzishwa mwaka 2017 kwa lengo la kupanua wigo wa mazao ya utalii kijiografia kwa kuendeleza Sekta ya Utalii katika Mikoa ya Kusini.

Mradi huo unatekelezwa kupitia fedha za mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani Milioni 150 kutoka Benki ya Dunia.

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO MWAKA -2050 July 17, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Manispaa Kibaha aungana na wanamichezo jijini Tanga

    August 24, 2025
  • Timu ya Soka Manispaa ya Kibaha yaitandika Bila huruma Manyoni Dc

    August 18, 2025
  • CRDB Bank Yatoa msaada wa madawati 30 Viziwaziwa Sekondari, Kibaha Manispaa

    August 14, 2025
  • Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha yatoa mafunzo ya Utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka2023

    August 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

Hospitali ya rufaa Pwani
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa