Na Byarugaba Innocent,Morogoro.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde ametembelea vipando pamoja na mabanda ya mifugo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa sherehe za Maonesho ya nanenane kanda ya mashariki yanayofanyika kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Mkoani Morogoro kuanzia Julai 31,2022
Aidha, Mhandisi Munde ameridhishwa na maendeleo yaliyopo kwani maandalizi hayo yametangazwa kufanyika ndani ya kipindi kifupi.
Pamoja na Mambo mengine amewapongeza waandaji wote hususan Mkuu wa Idara ya Mifugo Joseph Njau na Mkuu wa Idara ya Mifugo Charles Marwa kwa kupambana mpaka kuwa na sura ya kushiriki na kushindana.Mkuu wa Idara ya Kilimo ameeleza changamoto zaaandalizi hayo kuwa ni kutokuwepo kwa maji muda mwingi hali inayosababisha kutofikia lengo na matarajio kwani maji yangekuwepo siku zote vipando vingekuwa katika hali bora zaidi.Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo Charles Marwa ameeleza changamoto ya uchakavu wa jengo la halmashauri linalotumika kuoneshea mazao na bidhaa nyingine kuwa kwa Sasa limepoteza hadhi hivyo linahitaji maboresho madogo.
Kutokana na mwonekano wa jengo lenyewe kupoteza ladha, Mhandisi Munde ameridhia kuboreshwa kwa kupaka rangi na kurekebisha mfumo wa umeme ambao ni hatari ukizingatia kwa Sasa watafika watu wengi hivyo inaweza kuhatarisha maisha yao.
Maonesho ya nanenane kanda ya mashariki hujumuisha halmashauri zinazotoka kwenye Mikoa ya Dar-es-Salaam,Pwani, Morogoro na Tanga.
Kauli mbiu ya Maonesho ya sherehe za nanenane Mwaka,2022 zina kauli mbiu isemayo;Agenda 10/30 Kilimo ni biashara;Shiriki kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Haki Zote Zimahifadhiwa