• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MRADI WA TACTIC MANISPAA YA KIBAHA KUONGEZA FURSA ZA UCHUMI KWA WANANCHI

Posted on: September 25th, 2025

*

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA ) inatarajia kuleta manufaa makubwa kwa Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani na Miji mingine nchini, kupitia Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) ukitajwa kuongeza fursa za ajira kwa Vijana na kuchochea uchumi wa Manispaa ya Kibaha chini ya Maboresho makubwa ya mazingira ya ufanyaji wa biashara yatakayofanyika.


Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Septemba 25, 2025 katika Soko la Mnarani, Kibaha na Mhandisi Emmanuel Manyanga, Muwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TARURA ambaye pia ni mratibu msaidizi wa mradi wa TACTIC wakati wa utiaji saini Mkataba wa mradi wa TACTIC kwa Manispaa ya Kibaha ukihusisha Uboreshaji wa Miundombinu ya Barabara, Soko kuu la Mnarani, Bustani ya Mapumziko na burudani pamoja na ujenzi wa Jengo la Usimamizi wa mradi ukigharimu shilingi Bilioni 19.83 bila jumuisho la kodi ya ongezeko la thamani (VAT).


"Mradi huu kwa Manispaa ya Kibaha utaongeza fursa za ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuboresha hali za biashara katika maeneo husika na hivyo kuchangia maendeleo ya muda mrefu ya jamii na Taifa kwa ujumla. Pia huduma za usafiri na usafirishaji zitarahisishwa pamoja na  kupendezesha Manispaa hiyo inayokua kwa kasi na kuipa hadhi inayostahili," amesema Mhandisi  Manyanga.


Aidha alieleza kuwa Mradi wa Uendelezaji Mji wa Kibaha kwa awamu ya kwanza uliosainiwa leo unatekelezwa na Mkandarasi M/s Dimetoclasa Real Hope Limited kwa gharama ya shilingi 19, 832, 922, 855.99, ukitarajiwa kutekelezwa kwa miezi 15 na unahusisha ujenzi wa barabara za Tughe-Anglikana (Km 1.1), Barabara ya picha ya ndege- Hospitali ya Lulanzi (Km 3.7) pamoja na ujenzi wa Soko la Mnarani. Pia mradi utajenga bustani ya kisasa pamoja na jengo la usimamizi na uratibu wa Mradi.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge ametoa Wito kwa Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani kuitunza miundombinu inayotekelezwa na Mradi wa TACTICS akielekeza Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha kufanya tathmini ya miradi yenye kujiendesha yenyewe ikiwemo Masoko na Vituo vya Mabasi ili kuhakikisha miradi hiyo inatumika kuboresha huduma na kuongeza mapato ya Halmashauri na Serikali.


"Ni matarajio yetu sote kuwa miradi hii italeta mabadiliko chanya kwa Wananchi wa Manispaa yetu ya Kibaha na wageni ambao watafaidi huduma za mahitaji mbalimbali ya usafiri na usafirishaji, manunuzi ya vyakula, mavazi pamoja na mazingira bora ya kibiashara kwani ni dhahiri kuwa thamani ya maeneo husika itapanda na hivyo kusababisha ongezeko la mapato kwa Halmashauri yetu,” alisema Kunenge.


Aidha Mhe. Kunenge ametoa rai kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa haraka, ubora uliokusudiwa na kukamilika kwa wakati kwa mujibu wa mkataba na mpango kazi uliokubalika ili wananchi waanze kunufaika na miundombinu hiyo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza katika Manispaa ya Kibaha.


Mradi wa TACTIC ni mojawapo ya miradi inayofadhiliwa na serikali kuu kupitia Mkopo wa Benki ya dunia wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 410 bila VAT, malengo ya mradi huu yakiwa kuboresha miundombinu ya Miji 45 ya Tanzania pamoja na kujengea uwezo   Halmashauri ili ziweze kujiimarisha katika usimamizi wa uendelezaji Miji pamoja na ukusanyaji wa mapato.

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO MWAKA -2050 July 17, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Rc pwani aitaka Taasisi ya Elimu ya watu wazima kuleta matokeo chanya Sasa.

    October 02, 2025
  • Wazee 160 Mtaa wa Uyaoni waadhimisha siku ya wazee Duniani Kwa kupima Afya zao

    October 01, 2025
  • MRADI WA TACTIC MANISPAA YA KIBAHA KUONGEZA FURSA ZA UCHUMI KWA WANANCHI

    September 25, 2025
  • Wajasiliamali wadogo wanaopanga biashara zao pembeni mwa Barabara wamshukuru na kumpongeza Mkurugenzi Manispaa ya Kibaha

    September 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

Matangazo Mubashara Hafla ya Utiaji Saini mikataba ya Soko la Mnarani na miundombinu ya Barabara
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa