Anzeni utekelezaji wa mafunzo Mara moja. mwl. Isihaka Mwalimu.
Mbeya, Tanzania – Mratibu wa Mapato wa Manispaa ya Kibaha, Mwl. Isihaka Rashid Mwalimu, amewataka watendaji wa kata kutoka Manispaa hiyo kuanza mara moja kutekeleza kwa vitendo mafunzo wanayopatiwa katika Jiji la Mbeya.
Akizungumza akiwa jijini Mbeya, Mwl. Mwalimu amesema kuwa ni muhimu kwa watendaji hao kuanza kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha Manspaa ya Kibaha unakuwa safi, huku wakibuni mbinu za kuongeza mapato ya Manispaa.
“Unapojifunza ni lazima kuwe na mabadiliko. Mafunzo haya si ya kuyahifadhi tu bali ni kwa ajili ya kubadilisha namna tunavyofanya kazi. Tunapomaliza hapa, tunarejea vituoni tukiwa tayari kuendelea na kazi kwa kasi mpya, siyo kuanza upya,” alisema Mwl. Mwalimu.
Aidha, amesisitiza kuwa utekelezaji wa mafunzo kwa vitendo ni hatua muhimu katika kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Kibaha, akiongeza kuwa mabadiliko ya kiutendaji yanapaswa kuonekana mara moja baada ya mafunzo hayo.
Aidha amempongeza mtendaji wa wa Kata ya Misugusugu Fatuma Muna, ambaye ameanza utekelezaji Kwa kupiga simu na kuwajulisha watendaji wake wawahamasishe Wananchi juu ya utunzaji wa Mazingira.
Haki Zote Zimahifadhiwa