Kibaha, Pwani – Lina Joseph Kinabo, mfugaji mwenye umri wa miaka 67 kutoka Kata ya Tumbi, Manispaa ya Kibaha, ni miongoni mwa wafugaji waliothibitisha kuwa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa wa ndani unaweza kuwa chanzo kikubwa cha kipato na maendeleo ya kiuchumi.
Kwa sasa, Bi Kinabo anamiliki ng’ombe 28 wa maziwa, na ng'ombe mmoja ana kilo 800.Kupitia jitihada zake na matumizi ya maarifa ya kisasa katika ufugaji, amefanikiwa kujipatia mshahara wa kila mwezi wa shilingi 200,000, huku biashara yake ya maziwa ikimpatia faida ya kati ya shilingi milioni 2 hadi 3 kwa mwezi.
Mbali na kipato hicho, Bi Kinabo pia huwaajiri vibarua wa kudumu na wa muda, na amekuwa chachu ya maendeleo katika jamii yake, akiwasaidia vijana na wanawake kujifunza mbinu bora za ufugaji.
Kutokana na mafanikio yake, Bi Kinabo amekuwa mfugaji wa mfano katika maonyesho ya kilimo ya Nanenane, ambako hualikwa kutoa mafunzo kwa wafugaji wengine kuhusu namna ya kuboresha uzalishaji wa maziwa, afya ya mifugo, na uendeshaji wa ufugaji kama biashara endelevu.
“Ufugaji si kazi ya kubahatisha. Ukiweka juhudi na maarifa, unaweza kuishi maisha ya heshima. Ng’ombe wamenibadilishia maisha – na sasa nawatia moyo wenzangu, hasa vijana, kuingia kwenye sekta hii yenye tija,” alisema Bi Kinabo.
ameishukuru serikali Kwa kumpa mafunzo yanayomsaidia kuboresha maisha yake, na kutoa wito Kwa Jamii kujikita kuwekeza katika mifugo wa kuwa inalipa na inakufanya upate Afya Bora na kipato.
Haki Zote Zimahifadhiwa