• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Rais DKT SAMIA SULUHU HASSAN kuzindua Bandari kavu ya kwala na miradi ya miundombinu Pwani.

Posted on: July 22nd, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Bandari Kavu ya Kwala, Mkoani Pwani, Julai 31, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 22, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Abubakar Kunenge, amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo kubwa la kihistoria.

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Samia atazindua rasmi safari za Treni ya Mizigo kwa njia ya Reli ya Kisasa (SGR), kupokea mabehewa ya mizigo kwa njia ya Reli ya Zamani (MGR), pamoja na kuzindua Kongani ya Viwanda ya Kwala (Kwala Industrial Park), moja ya maeneo ya viwanda makubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Mhe. Rais atafanya uzinduzi rasmi wa safari za treni ya mizigo ya mwendo kasi kupitia Kituo Kikuu cha Kuunganishia Mabehewa ya Mizigo na Karakana ya Treni za Mizigo (Marshalling Yard) kilichopo Kwala,” alisema Mhe. Kunenge.

Aliongeza kuwa uzinduzi huo ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwekeza kwenye miundombinu ya kisasa ya viwanda, reli na bandari ili kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya uchumi.

Kuhusu Bandari Kavu ya Kwala, Mhe. Kunenge alisema kuwa mradi huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia wastani wa makasha ya mizigo 823 kwa siku, sawa na makasha 300,000 kwa mwaka. Hii itasaidia kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa asilimia 30.

Akifafanua zaidi, alisema kuwa Mhe. Rais Samia atapokea jumla ya mabehewa 160 ya mizigo, ambapo mabehewa 100 ni mapya yaliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya MGR, mabehewa 20 yamefanyiwa ukarabati, na mengine 40 yametolewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).

Kwa upande wa Kongani ya Viwanda ya Kwala, ambayo ni miongoni mwa maeneo ya viwanda makubwa zaidi Afrika Mashariki, Mhe. Kunenge alisema kuwa Mhe. Rais atazindua viwanda saba vilivyokamilika na vinavyoendelea na uzalishaji, pamoja na viwanda vitano ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Kongani hiyo inatarajiwa kuwa na zaidi ya viwanda 250.

Hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa, huku Mhe. Rais akitarajiwa pia kufanya mkutano mkubwa na wananchi mara baada ya shughuli za uzinduzi kukamilika.

Miradi inayotarajiwa kuzinduliwa inaonyesha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha sekta ya uchukuzi na usafirishaji, na kuifanya Kwala kuwa kitovu cha biashara na uchukuzi wa kimataifa (International Logistic Hub).

Aidha uzinduzi huo utaleta manufa makubwa yakiwemo kuongeza mapato, kukuza usafiri wa Reli, kupunguza uharibifu wa barabara, kutunza manzingira na kuongeza ushindani wa kikanda na Ushirikiano wa kikanda  na nchi za jirani kama vile DRC, Zambia, Rwanda,Burundi, Malawi, Zimbabwe, Uganda, na Sudani ya Kusini.

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO MWAKA -2050 July 17, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Azindua Rasmi Bandari kavu ya Kwala

    July 31, 2025
  • Matangazo ya mapokezi ya mabehewa mapya na yaliyokarabatiwa ya Mgr na ufunguzi wa Bandari kavu ya Kwala

    July 31, 2025
  • Rais Samia Kuzindua Usafirishaji wa mizigo Kwa SGR na Bandari ya KWALA Pwani.

    July 30, 2025
  • Kiwanda Cha Simenti chatoa Msaada wa Tsh milioni 36 Shule ya Msingi Misugusugu.

    July 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mansipaa ya Kibaha inakuletea television mtandao
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa