REDESO NA MKAKATI WA MATUMIZI YA NISHATI SAFI NA SALAMA TANZANIA
Na Byarugaba Innocent, Kibaha
Shirika lisilo la Kiserikali la Relief to Development Society (REDESO) linaendesha Mafunzo ya Matumizi ya Nishati Safi na salama kwa makundi ya Mama lishe,wakulima wa mbogamboga na madereza wa bodaboda 250 yenye lengo la kubadili mtazamo wa Matumizi ya Nishati chafu kuunga Mkono jitihada za Serikali kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mafunzo haya yanaendelea kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kibaha yakilenga kuhama kutoka kwenye Matumizi ya Nishati chafu kwenda safi kwa gharama nafuu na endelevu kwa kutumia rasilimali zinazopatikana kwenye Mazingira husika.
Mkurugenzi Mtendaji wa REDESO Abeid Kasaizi amesema shirika limeanza na Kibaha Kata ya Mkuza ambapo asilimia 62 ya watu waliohojiwa kuhusu Nishati Safi wamekiri kutoitambua
Aidha, Kasaizi amesema lengo la kuchagua kundi la Vijana wanaojishughulisha na ujasilimia wa bodaboda ni kutaka kuwahamisha kutoka kwenye Matumizi ya mafuta na kwenda kwenye Matumizi ya gesi na umeme na kundi la Mama lishe ni kuwahamisha kutoka kwenye Matumizi ya Kuni na Mkaa kwenda kwenye Matumizi ya Majiko banifu yanayotumia Mkaa kidogo ama teknolojia nyingine rafiki ya Nishati Safi.
Mzumbe Mussa, Mtaalam wa Nishati Safi na salama ameeleza kuwa Nishati ni ile inayozalishwa kutokana na Vyanzo ambayo ni rafiki wa Mazingira,havichafui hewa,Maji na Ardhi ili kuepukana na madhara ya muda mrefu kwa Maendeleo endelevu huku akizitaja kuwa ni Nishati ya jua, upepo, Maji,Joto Ardhi na Nishati inayotokana na viumbe hai.
Debetria Dionizi amelipongeza shirika Hilo kwa kutoa Mafunzo hayo na kwamba yamekuja kwa wakati sahihi kwani Matumizi ya Nishati Safi yatamuepusha na madhara ambayo amekuwa akiyapata kiafya,kumpunguzia gharama za Manunuzi ya Kuni na Mkaa na kumwongezea kipato kwani Sasa chakula kitaiva na kuwafikia wateja kwa wakati na kutoa wito kwa Serikali kuweka ruzuku kwenye Manunuzi ya gesi
Mkurugenzi wa REDESO Abeid Kasaizi taasisi yake yenye ufadhiri kutoka International Development Research Centre IDRC.CRDI ya nchini Canada itaendelea kutoa Mafunzo haya ili kuwafikia Watanzania wote kupitia vyuo vya VETA ikiwa ni kuunga Mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyetangazwa hivi karibuni kuwa Kinara na Mpambanaji wa Nishati safi na Salama Afrika
Haki Zote Zimahifadhiwa