Na Byarugaba Innocent,Lindi
Mke wa Rais wa awamu ya nne na Mbunge wa Jimbo la Mchinga,Mhe. Salma Kikwete ametoa rai kwa Kamati za kudhibiti VVU/UKIMWI nchini kufika Manispaa ya Lindi Kujifunza ili kuweza kukabiliana kwenye Maeneo yao.
Akitoa salaam kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Lindi na Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo kwa Kamati ya kudhibiti kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha kwenye kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi ya Meya wa Manispaa hiyo amesema amefurahishwa na Kamati ya Kudhibiti UKIMWI toka Kibaha Mji yenye kiwango cha Maambuzi asilimia 5.5 kufika Manispaa ya Lindi kujifunza kuwa ni sehemu sahihi kwani Wana maambukizi kidogo nchini kiwango cha 0.3 asilimia ukilinganisha na takwimu za Kitaifa kiwango cha 4.7 na kwamba iwapo kamati zote zitaongeza Kasi kwenye jambo hili uwezo wa kufikia asilimia sifuri upo.
Awali Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti UKIMWI kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Selina Msenga ameeleza kuwa takwimu za Kitaifa za hali ndogo ya Maambuzi ya VVU za Manispaa ya Lindi ndio kichocheo cha kwenda kwani pamoja na kuwa Mikoa yote miwili ipo kwenye ukanda wenye Mazingira yanayoshabihiana kwa kiasi kikubwa lakini Kibaha maambukizi yapo juu hivyo wamefika kupat a Uzoefu na maarifa mapya ya namna ya kukabiliana nayo.
Mratibu wa UKIMWI Manispaa ya Lindi yenye kata 32 na wakazi 278,800 Dkt.Zulfa Msumi amesema kuwa mafanikio yao yametokana na ushirikiano wa Halmashauri na watu waishio na VVU kwa kuhakikisha KONGA inakuwa hai na kusaidia jamii katika uhamasishaji wa kupima VVU ili kufahamu hali za maambukizi
Aidha,ameongeza kuwa kati ya vituo vya afya 49 vya kutolea huduma za afya,27 vinatoa huduma za matunzo kwa wenye VVU (CTC) na vituo 40 vinatoa huduma ya kupunguza maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT) kwa kushirikiana na USAID AFYA YANGU na CSSC/Amref ambao ni wafadhili
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba ameipongeza Manispaa ya Lindi kwa ushirikiano uliopo kati ya Wabunge,Wahe.Madiwani,Menejimenti,watumishi na wananchi wote na kwamba mafanikio wanayopata kwenye kupunguza maambukizi ya VVU ni matunda yake yanayotafutwa na wengine kwenda kujifunza kwao
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amewapongeza Manispaa ya Lindi hasa kwa kujiongeza kutafuta wadau wa kuchagiza Kasi ya mapambano hivyo ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Kibaha kutafakari nje ya boksi na kujiongeza na kuongeza ubunifu wa kutafuta wadau watakaosaidia kwani kutegemea bajeti ya Halmashauri pekee haitoshelezi
Takwimu za maambukizi ya VVU nchini Tanzania zinaonesha kuwa Mkoa unaoongoza kwa maambukizi makubwa ni Njombe wenye asilimia 11.4 huku Mkoa wa Lindi ukiwa na maambukizi kidogo ya asilimia 0.3
Haki Zote Zimahifadhiwa