Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Septemba 30,2023 Halmashauri ya Mji Kibaha itakabidhiwa mradi mkubwa wa Soko la kisasa kutoka kwa Mkandarasi Kampuni ya Elerai lililosanifiwa kujengwa kwa shilingi za Kitanzania 8,000,000,000.00 ambapo Mkataba wa awali ulikuwa shilingi 7,298,549,844, kazi za nyongeza shilingi 204,873,960 na ongezeko la Kodi ya thamani (VAT) shilingi 496,576,196
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Protas Dibogo ameileza kamati ya Siasa Wilaya iliyopita kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 kuwa mradi unasimamiwa na Mhandisi mshauri M/S Luptan Consult na Consultancy Ltd kwa gharama ya Shilingi 352,407,000.00 pamoja na VAT Shilingi 294,410,000,kutoka kwa wafadhili UN-CDF na shilingi 57,997,000 ikiwa ni mapato ya ndani hivyo kufanya jumla ya Shilingi 8,352,407,000
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mwajuma Nyamka amemshukuru Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa na kwamba Ilani imetekelezwa vema
Mhandisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha Brighton Kisheo amesema kazi zilizobaki ni umaliziaji wa Kawaida ikiwemo kufunga miundombinu ya Maji,umeme na taka ambapo anaamini zitaisha kwa wakati
Katibu tawala Wilaya ya Kibaha Moses Magogwa ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kujenga soko la Kisasa Kibaha ambalo chanzo muhimu cha Mapato na ajira mpya kwa wananchi
..."taarifa za usanifu zinaonesha kutakuwa na ajira mpya 253 na Wananchi zaidi ya 2000 watapata huduma kwa siku na Halmashauri ikitegemea kupata Mapato takribani 450,000,000 milioni "..
Natoa rai kwa wataalam kuhakikisha ifikapo Septemba 30,2023 kando ya kukabidhiwa,utaratibu wa kuwapata wafanyabiashara uanze
Haki Zote Zimahifadhiwa