Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Jumla ya Shilingi 1,093,998,425 zimeidhinishwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kujenga shule mbili mpya za Sekondari kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha kupitia mradi wa SEQUIP ndani ya Mwaka wa fedha 2021/2022 ili kuwapunguzia mwendo wa takribani kilometa 18 waliotembea wanafunzi kusaka Elimu
Shule hizo mpya ni Viziwaziwa iliyotumia kiasi cha Milioni 565,000,000 ikihusisha nyumba za walimu na Shule ya Mbwate itakayotumia milioni 528,000,000 mpaka kukamilika kwake.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba ameendelea na utaratibu wake wa kuitembelea miradi ya Maendeleo ambapo ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa shule ya Mbwate kwani majengo yote yapo hatua nzuri yakiwa na ubora unaoendana na thamani ya fedha.
"Kuweni na vipaumbele ili shule ifunguliwe kwa kujenga miundombinu ya Msingi ili watoto waingie kusoma waachane na kutembea umbali mrefu.Hiyo ndio azma ya Rais Samia". .amesema Ndomba
Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Godfrey Mwaduma ameeleza kuwa jumla ya vyumba vya madarasa 16,Maabara 6,Maktaba 2,Majengo ya Utawala 2 pamoja na miundombinu ya Vyoo na Maji inatosheleza kuanza kwa masomo kwenye shule hizo
Rosemary Msasi,Afisa Elimu Sekondari wa Kibaha Mji amesema Mhe.Samia Suluhu Hassan ametimiza ndoto yake ya kuwasaidia wanafunzi kwani shule hizo zitapunguza umbali wa kutembea kwa kilometa 18 kwa wanafunzi wa Mbwate kwenda Shule ya Miembesaba,kupunguza Msongamano kwenye shule kongwe ya Nyumbu,Kuongeza ufaulu pamoja kupunguza tatizo la mdondoko wa masomo na Mimba zisizo tarajiwa.
Haki Zote Zimahifadhiwa