Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Jumla ya milioni 181.5 zilizoidhinishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan zimekamilisha ujenzi wa Zahanati ya kisasa itakayowahudumia zaidi ya Wananchi 14,326 wa Mitaa ya Saeni,Jonung'a,Zogowale na Misugusugu Halmashauri ya Mji Kibaha.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Protas Dibogo ameeleza kuwa fedha hiyo inahusisha shilingi 75,000,000.00 kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri,Milioni 100,000,000.00 Serikali huku milioni 6,500,000.00 zikitolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mhe.Silvestry Koka kupitia Mfuko wa Jimbo.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dr.Peter Nsanya amesema kuwa jumla ya Chupa 12 za damu zimetolewa na Wananchi 12 walioshiriki kwenye Sherehe za ufunguzi wa Zahanati hiyo kati wananchi 265 waliopata huduma zikiwemo za saratani ya shingo ya mlango wa kizazi,tezi dume,ushauri nasaha na mpangilio mzuri wa ulaji ili kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambuliza kama shinikizo la damu.
Akizindua Zahanati hiyo Mhe.Silyvestry Koka amesema hayo ni mafanikio makubwa ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuwapa wananchi Maendeleo ikiwemo sekta ya Afya,Elimu,Miundombinu,Maji na mengineyo ili kuwaweka karibu na Serikali yao.
Aidha,amesema kuwa ushirikiano mkubwa anaopata kutoka kwa baraza la Madiwani na Wananchi wa Kata ya Misugusugu imekuwa ikimpa nguvu ya kuendelea kupambana kuwaletea Maendeleo kwani huo ni utelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025
Mhe.Koka ametumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa propaganda zinazoendelea za kumdhoofisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia kuwa ameuza Ardhi na Bandari kwa DP-World wazipuuze na kamwe Serikali haiwezi kufanya hivyo.
..."Bandari kwa miaka 20 ilikuwa ikiendeshwa na TICKS,haikufanya vizuri Sasa Serikali inataka kumpa mwekezaji atakayeiendesha kwa tija.Je,Hilo ni jambo baya?"..... aliwauliza wananchi ambao walijibu hapanaaa kwa vigelegele ,shangwe na nderemo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha amemshukuru Mhe.Koka kwa namna alivyopambana Zahanati na miradi mingine inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Jimbo la Kibaha Mjini.
Ametoa rai kwa wananchi wote kuendelea kumuunga mkono ili akamilishe ahadi zote alizoahidi wakati akiomba kura.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka amewaomba wananchi kuendelea kushikamana na Kuiamini CCM kwani imeendelea kuwaletea Maendeleo.
Haki Zote Zimahifadhiwa